Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Chadema, ACT waungana, watoa tamko zito la Uchaguzi Mkuu
Habari za SiasaTangulizi

Chadema, ACT waungana, watoa tamko zito la Uchaguzi Mkuu

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema
Spread the love

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na ACT-Wazalendo vimeomba kuitishwa upya Uchaguzi Mkuu wa Urais, wabunge, wawakilishi na madiwani, kwa maelezo kwamba havikubaliani na matokeo ya Uchaguzi wa tarehe 28 Oktoba, 2020. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Tamko la msimamo limetolewa leo tarehe 31 Oktoba, 2020 jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe.

“Kwa umoja wetu tunaamini kilichofanyika katika uchaguzi wa tarehe 28 Oktoba, 2020 hakina sifa wala uhalali wa kuitwa Uchaguzi Mkuu bali ni unyang’anyi na uporaji wa kutumia nguvu dhidi ya haki ya Watanzania kuchagua viongozi wanaowataka,” amesema Mbowe.

Aidha, Mbowe amesema vyama hivyo vinaagiza Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania (NEC) na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), kuvunjwa na kuundwa tume huru itakayosimamia uchaguzi huo.

“Tunadai kuitishwa upya kwa Uchaguzi Mkuu haraka iwezekanavyo. Tunahitaji kuvunjwa ZEC na NEC kuundwa tume huru ya uchaguzi itakayosimamia uchaguzi huo,” amesema Mbowe.

Zitto Kabwe, Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo

Kwa upande wake Kiongozi Mkuu wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amesema chama chake kinaunga mkono msimamo huo, na kuwaomba Watanzania kuchukua hatua kupinga matokeo ya uchaguzi huo.

Aliyekuwa Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chadema, Tundu Lissu amesema “Mimi nawataka wananchi wetu wachukue mamlaka yao tena. Kuhakikisha hayo matokeo ya uchaguzi yanabadilishwa ili tuwe na uchaguzi wa kutoa mamlaka kutoka kwa wananchi kwenda kwa wawakilishi wao mbalimbali.”

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!