December 2, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Tundu Lissu azungumzia ushindi wa Dk. Magufuli

Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti Chadema

Spread the love

ALIYEKUWA Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu amezungumzia ushindi wa Mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 28 Oktoba 2020 na kusema aliyajua mapema. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Jana tarehe 30 Oktoba 2020 Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania (NEC) ilimtangaza Dk.  Magufuli kuwa Rais mteule wa Tanzania, baada ya kupata kura milioni 12.5 kati ya milioni 15.9 zilizopigwa huku Lissu akipata kura milioni 1.9.

Akizungumzia matokeo hayo, Lissu amesema aliyatambua mapema. Huku akisistiza kuwa matokeo hayo hayakuwa halali kutokana na dosari zilizojitokeza kwenye uchaguzi huo.

“Magufuli hajashinda uchaguzi huu. Unakumbuka katika mkutano wangu wa kampeni tulisema kwamba tulikuwa na taarifa ya kwamba kulikuwa na kura za Magufuli na nilitamka ni milioni 12 na kura ambazo tume imezitangaza za Magufuli amepata ni milioni 12.5,” amesema Lissu.

Rais John Magufuli

Lissu amesema ushindi huo una dosari kwa madai kuwa matokeo yake yamesababisha Taifa kuwa na dalili za msiba kila mahali badala ya furaha na shamrashamra za ushindi.

“Walioshinda uchaguzi wa haki si huwa wanashangalia lakini kwa nini kuna dalili ya msiba? Kila mahali msiba wa Taifa sababu kila mtu anajua kwamba ushindi haukuwa wa haki,” amesema Lissu.

Wakati huo huo, Chadema na Chama cha A T-Wazalendo vimetangaza kutotambua matokeo ya uchaguzi huo, yaliyokipa ushindi wa kishindo wa CCM.

error: Content is protected !!