Thursday , 18 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Chadema, ACT-Wazalendo wapinga matokeo ya uchaguzi Tanzania
Habari za Siasa

Chadema, ACT-Wazalendo wapinga matokeo ya uchaguzi Tanzania

Spread the love

VYAMA viwili vikuu vya upinzani nchini Tanzania – Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kile cha ACT-Wazalendo – vimepinga matokeo ya uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani uliofanyika tarehe 28 Oktoba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Kwa mujibu wa tamko la pamoja la viongozi wakuu wa vyama hivyo, lililotolewa jijini Dar es Salaam, leo Jumamosi, uchaguzi mkuu uliyoisha, ulitawaliwa na mizengwe, hila, ghiriba na udanganyifu.

Wakizungumza na waandishi wa habari, makao makuu ya Chadema, viongozi hao wamesema, vinapinga matokeo ya uchaguzi wa Jumatano iliyopita, yaliyomtangaza rais aliyeko madarakani, John Magufuli, kuwa mshindi, kwa kuwa ”kilichofanyika si uchaguzi, bali ni unyang’anyi wa demokrasia.”

Aidha, kufuatia uamuzi huo wa kutotambua matokeo ya uchaguzi, vyama hivyo vimeitisha maandamano ya nchi nzima ili kudai kurejewa kwa uchaguzi huo.

Chama cha Wananchi (CUF) kimetangazwa kushinda ubunge katika Jimbo la Mtwara Vijijini.

Amesema, licha ya ushindi huo, vyama hivyo haviutambui kwa kuwa sio halali na kwamba  haviko tayari kuhalalisha matokeo ambayo si halali.

“Sisi kama vyama tumesema uchaguzi huu hatuutambui na tunapoacha kutambua tumeridhishwa pasipo shaka matokeo yoyote hata kama yametoa nafasi katika chama chetu sio halali, yametengenzewa kwa mkakati kutugawa,” amesisitiza Mbowe.

 

Ameongeza, “sisi hatutakubali kuwa washirika kwa mapato ya jinai hatutashiriki kufaidi matunda ya uhalifu. Sisi madiwani waliotangazwa wa Chadema na ACT hatuwatambui, uchaguzi huu na  matokeo yoyote hata kama yanatoa upendeleo kwa vyama vyetu hatuyatambui.”

Mkutano huo wa waandishi wa habari ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali wakuu wa vyama hivyo, akiwamo mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe; katibu mkuu, John Mnyika na Kiongozi Mkuu wa ACT-Wazalendo, Zitto Zuberi Kabwe.

Wengine, ni makamu mwenyekiti wa ACT- Wazalendo (Bara), Doroth Semu; aliyekuwa mgombea urais wa Muungano, Tundu Lissu; mgombea wake mwenza, Salum Mwalimu na aliyekuwa mgombea ubunge katika jimbo la Kinondoni (ACT- Wazalendo), Saed Kubenea.

Akizungumza katika mkutano huo, Mbowe amesema, “uchaguzi ulioendeshwa na ZEC (Tume ya Uchaguzi Zanzibar) na NEC (Tume ya Taifa ya Uchaguzi), haukuwa huru na haki,” na kuongeza, “Chadema na ACT-Wazalendo, hawakubaliani na mwenendo wa uchaguzi na matokeo yake.”

Zitto Kabwe, Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo

Amesema, “uchaguzi huu hatuutambui na tunapoacha kutambua tumeridhishwa pasipo shaka matokeo yoyote hata kama yametoa nafasi katika chama chetu sio halali, yametengenzewa kwa mkakati kutugawa.”

Miongoni mwa madai yao, ni kuzitaka mamlaka za nchi, kuzivunja NEC na ZEC na kuitishwa uchaguzi mwingine mpya haraka iwekezekanavyo.

Mbowe amesema, vyama hivyo viwili, vinawaomba wanachama wake na na wote wasiokubaliana na kilichotokea, “kushiriki katika maandamano ya amani ya kuanzia 2 Novemba 2020 hadi hapo madai yetu yakapotelekezwa.”

Kupatikana kwa taarifa za kupinga matokeo ya uchaguzi huo, kumekuja siku tatu tangu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo ambaye pia alikuwa mgombea wa urais wa Zanzibar, Maalim Seif Seif Sharif Hamad, kukamatwa pamoja na viongozi wengine wa chama hicho.

Maalim Seif na wenzake, walikamatwa muda mfupi baada ya kutangaza maandamano kupinga matokeo ya uchaguzi huo. Aliachiwa huru muda mfupi baadaye, huku baadhi ya viongozi akiwamo Ismail Jussa Radhu.

Tundu Lissu, aliyekuwa Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chadema

Katika uchaguzi huo, matokeo yaliyotangazwa na NEC na ZEC, yanaonyesha kuwa Chadema kimeambulia jimbo moja la Nkasi Kaskazini, lililochukuliwa na Aidah Khenani, huku ACT – Wazalendo, kimeambulia viti vitatu vya ubunge na vinne vya uwakilishi, kisiwani Pemba.

Nacho Chama cha Wananchi (CUF), kimetangazwa kushinda ubunge katika jimbo la Mtwara Vijijini.

Kuhusu wabunge wake kushiriki vikao vya Bunge na kuteuwa wabunge wa Viti Maalum, Mbowe alisema, “sisi hatutakubali kuwa washirika kwa mapato ya jinai hatutashiriki kufaidi matunda ya uhalifu. Sisi madiwani waliotangazwa wa Chadema na ACT hatuwatambui, uchaguzi huu na matokeo yoyote hata kama yanatoa upendeleo kwa vyama vyetu hatuyatambui.”

Kwa upande wake, Zitto amesema, hawakubaliani na matokeo ya ushindi huo kwa kuwa hakukuwa na uchaguzi huru na wa haki.

Amesema, kutokana na dosari zilizojitokeza, wanaomba uchaguzi huo urudiwe upya.

Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, ZEC ilifuta uchaguzi wote wa rais Zanzibar, wawakilishi na madiwani, katikati ya kipindi ambacho wawakilishi walishatangazwa washindi na kukabidhiwa vyeti vyao.

Wakati hayo yakiendelea, Lissu amezitaka jumuiya ya kimataifa kutotambua viongozi waliopatikana katika uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu.

Alhamisi iliyopita, Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania, ulizitaka mamlaka za taifa hilo la Afrika Mashariki, kushirikiana na wadau mbalimbali kushughulikia kwa uwazi malalamiko yanayotolewa kuhusu uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 28 mwaka huu.

Ubalozi huo kupitia tamko lake lililotolewa tarehe 29 Oktoba 2020, umeeleza kuwa kufanya hivyo kutarejesha imani na kutekeleza azma ya kuheshimu utawala wa sheria na dhana ya utawala bora.

Moja ya malalamiko yaliyotajwa na ubalozi huo ni kuhusu uwepo wa kura feki katika uchaguzi huo.

2 Comments

  • Mnawashwa nyie…KAPANULIWENI TAKO..si mlikula hela za mabeberu kwa ahadi ya kushinda uongozi?
    Watz wamewapiga chini..saivi hakuna namna ya kulipa mihela ya watu zaidi ya KUPANULIWA TAKO NA KUPACHIKWA KIGOGO CHA MZUNGU.

  • kutumika kubaya sana. wewe unaetukana hapa unatumika na wanaume zako wa ccm, hujitambui wala hujielewi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

Regina Mkonde: CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia kutunukiwa udaktari wa heshima Uturuki

Spread the loveBaraza la Chuo Kikuu cha Ankara, ambacho ni cha pili...

error: Content is protected !!