TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imemtangaza Dk. John Magufuli wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa Rais mteule wa Tanzania baada ya kupata kura milioni 12.5 kati ya milioni 15.9 zilizopigwa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Akitangaza matokeo hayo leo Ijumaa tarehe 30 Oktoba 2020, Mwenyekiti wa NEC, Jaji Semistocles Kaijage amesema, waliojiandilisha kupiga kura walikuwa milioni 29.
Amesema, waliopiga kura katika uchaguzi mkuu uliofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020 walikuwa milioni 15.9.
Jaji Kaijage amesema, kura halali zilikuwa milioni 14.8. Mwenyekiti hiyo amesema, Tundu Lissu wa Chadema amepata kura milioni 1.9.

Jaji Kaijage amesema, Jumapili tarehe 1 Novemba 2020, itafanyika shughuli ya kukabidhi hati ya ushindi kwa Dk. Magufuli na mgombea wake mwenza, Samia Suluhu Hassan.
Katika uchaguzi mkuu uliomwingiza Magufuli madarakani mwaka 2015, Dk. Magufuli alipata kura milioni 8.88 sawa na asilimia 58.46 huku mshindani wake, Edward Lowassa wa Chadema alipata kura milioni 6.07 sawa na asilimia 39.97
Leave a comment