Tuesday , 7 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Maalim Seif: Sasa imetosha
Habari za Siasa

Maalim Seif: Sasa imetosha

Maalim Seif Sharif Hamad, aliyekuwa Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo
Spread the love

MAALIM Seif Shariff Hamad, mgombea urais visiwani Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, amesema uvumilivu sasa imetosha. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Amesema, tofauti na chaguzi zilizopita, uchaguzi wa safari hii hatomzuia mtu yeyote kujitokeza na kutetea haki yake.

Maalim Seif ambaye ni mwenyekiti wa chama hicho, ametoa kauli hiyo leo Jumanne tarehe 20 Oktoba 2020, baada ya mwandishi wa habari kumuuliza, kama atafanya tofauti gani na miaka mingine ambayo amekuwa akilalamika kusinda na kupokwa ushindi.

“Siku zote tulikuwa tukitahadharisha kwa kudhani wenzetu ni waungwana. Kwamba, wenzetu watatilia maanani tunayozungumza na siku zote mimi niseme, nilikuwa nawazuia watu wasiingie barabarani, nyote mnajua. Mwaka huu simzuii mtu, atakayeamua kufanya lolote kutetea haki yake, simzuii. Kwa hiyo, ngojeni muziki tarehe 27 na 28 Oktoba mtauona,” amesema Maalim Seif.

Maalim Seif Sharrif Hamad, Mgombea Urais Zanzibar kwa tiketi ya ACT-Wazalendo

“Tuiache demokrasia ifuate mkondo wake kwa amani. Tumekishwavumilia vya kutosha, sasa tunakwenda tarehe 27 na tarehe 28 Oktoba tukiwa tayari kwa lolote lile litakalotokea. Kulinda demokrasia na kulinda haki ya Wazanzibari kumchagua rais wanayemtaka.”

Amesema, katika uchagzi wa mwaka huu, Wazanzibar hawawezi kuvumilia haki yao kuporwa na kwamba, tayari wameishapitia mengi katika maisha yao.

“Nataka kutahadharisha kuwa Wazanzibar wamedhamiria kulinda demokrasia, katu hatukubali kuendelea kudharauliwa. Wazanibar wameishapitia mengi, wamevuta subira na uvumilivu mkubwa na kupigiwa mfano. sasa imetosha.”

“Nchi yetu tuliamua kwa hiyari kuingia katika mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, jambo hili lipo katika Katiba ya Taifa letu, Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Katiba ya Zanzibar. Tunalazimika kusimamia Katiba zetu kwa maneno na vitendo,” amesema.

Kiongozi huyo nguli Zanzibar, amelalamikia baadhi ya mambo ikiwemo kutoridhishwa na daftari la wapiga kura, baadhi ya Wazanzibari kutojumuishwa kwenye daftari hilo.

Akizungumzia kura ya mapema, Maalim Seif amedai, yeye na chama chake hakikubaliana na uamuzi wa kura ya mapema inayowataka wafanyakazi waanze kupiga kura kisha tarehe 28 Oktoba ndio wengine wakapige kura.

“Kura ya mapema, tunaambiwa lengo la kura hii ni kuwawezesha watu wenye majukumu ya ulinzi na usalama pamoja na wasimamizi wa uchaguzi kupata nafasi ya kusimamia shughuli za ulinzi na usalama siku ya uchaguzi mkuu.
“Tunajiuliza maswali mengi. Wazanzibari wanashiriki chaguzi mbili tofauti, kuna uchaguzi wa Zanzibar na ule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, sasa watumishi tunaambiwa kuwa wanatakiwa kupiga kura siku moja kable ya uchaguzi mkuu, hawa hawataruhusiwa kuchagua rais na wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?” amehoji Maalim Seif

“Uchaguzi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni siku moja tu, tarehe 28 Oktoba, ikiwa (watumishi Tanzania Bara) bado watapewa fursa ya kutumia haki yao siku hiyo hiyo, ipo wapi mantiki ya kuwepo kwa kura ya mapema Zanzibar tu?”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Jacob, Malisa wapandishwa kizimbani kwa mashtaka ya uongo mitandaoni

Spread the loveMKURUGENZI wa Shirika la Haki, Godlisten Malisa na mwanachama wa...

BiasharaHabari za Siasa

Bunge laitaka Serikali kudhibiti ufisadi miradi ya mkakati

Spread the loveKAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, imeitaka Serikali kuimarisha...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Wizara ya Uchukuzi yaomba kuongezewa bajeti na Bunge

Spread the loveWIZARA ya Uchukuzi imeliomba Bunge liidhinishe bajeti yake kwa mwaka...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali kutafuta mwekezaji mwingine Bandari ya Dar es Salaam

Spread the loveSERIKALI inaendelea kutafuta mwekezaji mwingine atakayeendesha gati namba nane hadi...

error: Content is protected !!