Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Hivi ndivyo Membe alivyomuunga mkono Lissu
Habari za SiasaTangulizi

Hivi ndivyo Membe alivyomuunga mkono Lissu

Spread the love

BERNARD Kamilius Membe, mgombea urais Tanzania kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, ni miongoni mwa wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya chama hicho, waliobariki kumuunga mkono Tundu Lissu, mbombea urais Tanzania kupitia Chadema. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne tarehe 20 Oktoba 2020, jijini Dar es Salaam, Maalim Seif Sharif Hamad ambaye ni mwenyekiti wa ACT-Wazalendo amesema, vikao vilivyopitisha azimio la kumuunga mkono Lissu, Membe alishiriki.

“Naye (Membe) akatuhakikishia tarehe kwamba, kama atakua hajaanza kampeni, basi anakubali tumuunge mkono Lissu. Hivyo, kamati ya uongozi kwa kauli mmoja akiwemo Membe tukakubaliana, tumuunge mkono Lissu,” amesema Maalim Seif.

Maelezo hayo ameyatoa baada ya mwandishi kutaka kujua msimamo wa chama chake kuhusu kauli ya Membe aliyoitoa jana Jumatatu tarehe 19 Oktoba 2020, kwamba yeye bado ni mgombea halali na ataendelea na kampeni zake.

Mwandishi alimweleza kwamba, yeye (Maalim Seif) na Zitto Kabwe ambaye ni kiongozi wa chama hicho, wameweka wazi, watampigia kura Lissu na kutaka wafuasi wa chama hicho kumuunga mkono mgombea huyo, tofauti na kauli ya Membe ambaye ‘ameapa’ kuendelea na kampeni zake za urais.

“Nataka kufunga bao dakika ya 89 kutokea benchi. Watanzania make macho na make chonjo. Tumefanya kazi huku chini, sasa tunakuja juu kupata bao la ushindi dakika ya 89 na dakika za nyongeza,” ni kauli ya Membe akisisitiza kuendelea na kampeni zake.

Maalim Seif ameeleza kusikitishwa na kauli hiyo na kwamba, uamuzi wa kumuunga mkono Lissu haukuwa wake binafsi wala wa Zitto bali ni wa vikau halali vya chama hicho.

“Niseme nasikitika sana kwa aliyozungumza ndugu yangu Membe jana. Chama chetu cha ACT-Wazalendo, kupitia mkutano mkuu wa Taifa, uliamua kwamba tunataka mabadiliko katika nchi yetu, na kama vyama makini havutashirikiana, itakuwa ni vigumu kuoindoa CCM.

“Kwa hivyo, Mkutano Mkuu wa Taifa ukatoa madaraka kwa Halmashauri Kuu, Kamati Kuu na Kamati ya Uongozi kuhakikisha ACT-Wazalendo inafanya kila juhudi ili kuhakikisha tunashirikiana na wenzetu katika vyama ambavyo ni makini,” amesema Maalim Seif

“Na niwaambieni, ndugu Membe alipokuja kwenye chama chetu, tulimwambia mapema kabisa, maamuzi ya Mkutano Mkuu, tushirikianena vyama vingine. Je mwenzetu, unachukua nafasi hii tukiamua kushirikiana na vyama vingine, utakubali? akasema naam nitakubali.”

Hivyo, Maalim Seif amehoji waandishi kwamba, je wamemuona Membe akiendelea na kampeni za urais? “sasa embu niambieni mmeona kampeni ya Membe lini? mmeiona kampeni ya Membe, mmeiona?” ameohji.

Akizungumzia uamuzi wa kumuunga mkono Lissu, Maalim Seif amesema, uamuzi huo ulitokana baada ya kuona mgombea wake (Membe) hafanyi kampeni.

“Sasa niwaambieni, baada ya kuona kampeni zinaenda takribani wiki moja na nusu huku kampeni zetu zinasuasua tangu kutafuta wadhamini, kama viongozi tulikutana, tukashauriana na Membe akiwepo. Yeye ni Mjumbe wa Kamati ya Uongozi kwa sababu ni mshauri mkuu wa chama, tukashauriana mgombea wetu haonekani.”

“Nasikitika mjumbe wa kamati hiyo hiyo leo anakuja kukana! nasikitika sana. Ana dhamira gani? Mimi kama mwenyekiti wa chama na moja ya majukumu yangu ni kusimamia maamuzi ya vikao vya chama. Mimi ni lazima nisimamie maamuzi ya vikao vya juu vya chama,” amesema Maalim Seif.

Maalim Seif ametumia mkutano huo kuwataka wafuasi wa chama hicho kumuunga mkono Lissu katika ngazi ya urais Tanzania Bara huku akisisitiza, mwenye uwezo wa kumng’oa Dk. John Magufuli, mbombea urais wa CCM ni Lissu.

“Eembu niambieni kama mtakua fair (mtasema haki), ni mgombea yupi anaweza kumshinda Magufuli? Nani mwenye uwezekano wa kumshinda Magufuli? Ni Lissu. Na mimi niwaombe wanachama wenzangu haya ni maamuzi halali, lazima tufikirie nidhamu kwamba moja katika wajibu wa mwanachama ni kuheshimu maamuzi halali ya vikao halali vya chama.”

“Si kwamba hatumpendi Membe…nia yake ni kutaka kuwachanganya Watanzania tu lakini msimamo wa ACT-Wazalendo ni kuwa, mgombea anayeelekea kushinda ni ndugu Tundu Lissu,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

error: Content is protected !!