June 21, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Azam FC yajikita kileleni

Spread the love

KLABU ya Azam Fc imejikita kileleni kwenye msimamo wa Ligi Bara baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ihefu FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Mbeya … (endelea).

Mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya ulishuhudia Azam FC ikiiandika ushindi wa saba katika michezo saba waliocheza kwenye Ligi kuu Tanzania Bara.

Mabao ya Azam FC kwenye mchezo huo yalifungwa na Ayubu Lyanga 63 na Iddi Nado 70′ huku pasi zote za mabao zikitoka kwa Prince Dube.

Kwa matokeo hayo Azam FC sasa itakuwa inafikisha pointi 21 huku ikifuatiwa na Simba kwenye nafasi ya pili ikiwa na pointi 13 sawa na Yanga ambayo inashika nafasi ya tatu zote zikiwa na michezo miwili mkononi.

error: Content is protected !!