Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Michezo Barbara amrithi Senzo Simba
Michezo

Barbara amrithi Senzo Simba

Spread the love

MABINGWA wa soka Tanzania Bara, Simba imemtangaza Barbara Gonzalez
Kuwa Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) mpya. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es
Salaam…(endeleaa)

Barbara ametangazwa leo Jumamosi tarehe 5 Septemba 2020 na Mwenyekiti wa Bodi ya Simba, Mohamed Dewji ‘Mo’ kwenye mkutano wake na waandishi wa habari.

Barbara amechukua nafasi iliyoachwa wazi na Senzo Mazingiza alijiuzulu ghafla kisha kujiunga na watani zao Yanga.

Senzo ambaye ni raia wa Afrika Kusini, alitangaza kujiuzulu tarehe 9 Agosti 2020 na siku hiyohiyo akatimkia kwa watani zao Yanga yenye makao yake makuu Jangwani jijini Dar es Salaam.

Senzo Mazingiza, Aliyekuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba

Dewji amesema “Simba kwenye msimu huu 2020/21 tuna shabaha na shabaha yetu ni kuendelea kutetea ubingwa wa ligi kuu. Sisi tuna ndoto ya kufanya vizuri ili kushinda klabu bingwa Afrika.”

“Kocha anajua, wachezaji wanajua, wamejipanga na sisi tumejipanga, najua kutakuwa na ushindani mkubwa lakini sisi tumejipanga,” amesema Dewji

“Wanasimba tuendelee kutuunga mkono na kujitokeza uwanjani kuwapa nguvu wachezaji na Mungu akitujaalia tutaendelea kutetea ubingwa wetu. Shabaha yetu ni kufanya vizuri katika mashindano ya kimataifa. Mwaka jana ulikuwa na bahati mbaya ilitokea,” amesema.

“Tunataka kucheza mechi moja ya kirafiki nzuri kabla ya mashndano hayo na shabaha yetu ni kuingia kwenye makundi na tukishaingia kwenye makundi tunaanza kuzungumza mengine,” amejinasibu Dewji

Kuhusu CEO huyo mpya, Dewji amesema “ni msomi, mtu wa matendo na siyo mtu wa maneno mengi.”

Amesema, kikao cha bodi kilichokutana jana, Barbara alikuwa ana kaimu nafasi hiyo ambapo miongoni mwa agenda ni kumtafuta CEO mpya ambapo “bodi ilimpendekeza na wote wengine wamemuunga mkono.”

Dewji amemweleza Barbara kwamba, Simba ni Taifa kubwa, “hapa kuna presha na kuna mambo mengi mazuri na ya hovyo, lazima uwe na ngozi ngumu kupambana kwa kuendeleza ushindi wetu, falsafa yetu ya Simba.”

Kwa upanmde wake, Barbara amesema “Nashukuru wana Simba kwa ujumla na wana bodi kwa kunipitisha. Tumefanya kazi kwa miaka miwili mitatu ya mabadiliko na kwa wiki tatu mwezi nikikaimu.”

“Niko hapa kuendeleza malengo ya Simba, nitatoa ushirikiano mkubwa na tumejipanga,” amesema Barbara

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Europa na Conference kukupatia pesa ndefu leo

Spread the love  ALHAMISI ya leo tutaenda kushuhudia mitanange ya kukata na...

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

Michezo

Usiku wa Ulaya umerejea kibabe kabisa

Spread the love  LIGI ya Mabingwa barani Ulaya imerejea tena na awamu...

Habari MchanganyikoMichezo

Mambo ya Ndani, Ulinzi zang’ara michezo ya Mei Mosi Arusha

Spread the loveRais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA), Tumaini...

error: Content is protected !!