Monday , 27 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbatia atoa siri upinzani kutoungana uchaguzi mkuu 2020
Habari za Siasa

Mbatia atoa siri upinzani kutoungana uchaguzi mkuu 2020

Spread the love

JAMES Mbatia, Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi nchini Tanzania, amesema ukosefu wa uaminifu ndiyo sababu vyama vya siasa vya upinzani kutofikia mwafaka wa kuungana katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Mbatia aliyekuwa mwenyekiti mwenza wa vyama vilivyounda Umoja wa Katiba ya Wanachi (Ukawa) mwaka 2015, ametoa sababu hiyo leo Jumamosi tarehe 5 Septemba 2020 katika uzinduzi wa kampeni za NCCR-Mageuzi kwenye Viwanja vya Zakhiem- Mbagala jijini Dar es Salaam.

Mwanasiasa huyo amesema katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 vyama vya upinzani viliaminiana ndio maana viliungana kwa kusimamisha mgombea Urais mmoja na kuachiana majimbo, lakini katika uchaguzi huu vimeshindwa kutokana na kutoaminiana.

Ukawa ulikuwa ukiundwa na vyama vinne vya NCCR-Mageuzi, NLD, Chadema na CUF na mgombea urais alikuwa Edward Lowassa, Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania.

“Yaani hofu tu, nchi ya nani hii? Ukiangalia vyama vya siasa hofu tu na hii hofu inasababisha hakuna kuaminiana. Tujiulize kwa nini vyama vya siasa hatuaminiani tena? Je tatizo ni wewe Mbatia? Mwaka 2015 tulikuja na Edward Lowassa hapa (Zakhiem), leo havipo kwa nini usijiulize hatuaminiani. Nasema ukweli na mkweli ni mpenzi wa Mungu, hatuamiani,” amesema Mbatia.

Wenyeviti Wenza wa UKAWA, kutoka kushoto ni Freeman Mbowe (Chadema), Prof. Ibrahim Lipumba (CUF), James Mbatia (NCCR-Mageuzi) na Emmanuel Makaidi (NLD).

Mbatia amesema, ili hofu hiyo ya kutokuaminiana iishe, Tanzania inatakiwa ipate mwafaka wa kitaifa huku akiwaomba viongozi wa dini kusimamia upatikanaji wa mwafaka huo.

“Unaweza kumuona mtu anakuchekea lakini moyoni anaumia, unaweza kuona mtu anasema anakuombea lakini moyoni anaumia. Hata viongozi wetu wa dini, tunawaomba sio kutuombea tu mshiriki kwa pamoja kujenga mwafaka wa kitaifa,” amesema Mbatia.

Kuhusu uchaguzi mkuu, Mbatia amemuomba Jaji Semistocles Kaijage, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kuwasimamia watendaji wake wa ngazi za chini kutenda haki ili taifa libaki salama wakati wa uchaguzi na baada ya mchakato huo.

“Tume ya uchaguzi ya Jaji Kaijage na wenzako, wasimamie vizuri walioko chini watende haki, tunataraji baada ya uchaguzi walioshinda wapongezwe ili haki itende na hiyo itafanyika kama haki itatendeka. Huwezi kumaliza uchaguzi mnagombana tu, watoto wajifunze nini kwetu? Tugombane kwa ajili ya ubunge na udiwani” amehoji Mbatia.

Wakati huo huo, Mbatia ambaye ni mgombea ubunge wa Vunjo Mkoa wa Kilimanjaro amewataka wanasiasa na Watanzania kwa ujumla kuacha kiburi husuan katika kipindi cha kampeni za uchaguzi.

“Watanzania tuwe wanyenyekevu, tuache kiburi hasa walio madarakani wanaojiona bora kuliko wengine. Ulimi ni kiuongo kidogo lakini unaweza kuweka hai au kuuwa, inategemea vinywa vyetu tunatumiaje, naomba wanasiasa wote hasa wa NCCR Mageuzi kabla ya kusema chochote omba Mungu akutangulie sio unaenda kutukana tukana, unakejeli wenzako wengine,” amesema Mbatia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kasekenya aipa Tanroads wiki kukarabati barabara Morogoro

Spread the loveNaibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya ametoa wiki moja...

Habari za SiasaTangulizi

‘Aliyemtonya’ Lissu kuhusu rushwa arejea madarakani

Spread the loveMwenyekiti wa zamani wa Chadema Mkoa wa Iringa, William Mungai...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia: Tutaendelea kupigania malengo ya afrika

Spread the loveRais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema dhamira ya Tanzania...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

NHC yadai bil. 2.1 taasisi za Serikali, Waziri atoa maagizo

Spread the loveKAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii...

error: Content is protected !!