Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa 386 wajitosa majimbo tisa K’njaro, sita waingia mitini
Habari za Siasa

386 wajitosa majimbo tisa K’njaro, sita waingia mitini

Katibu wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, Jonathan Mabihya
Spread the love

WANACHAMA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) 386 kati ya 392 wamechukua na kurejesha fomu za kuomba chama hicho kiwapitishe kuwania ubunge katika majimbo tisa ya Mkoa wa Kilimanjaro. Anaripoti Mwandishi Wetu, Moshi…(endelea)

Wanachama sita waliochukua fomu hizo tangu walipoanza kuzitoa tarehe 14 hadi leo Ijumaa ya tarehe 17 Julai 2020 saa 10 jioni lilipofungwa, hawakuzirejesha.

Hayo yamesema na Katibu wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, Jonathan Mabihya wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Moshi baada ya kubitimishwa kwa shughuli hiyo.

Amesema kati ya wanachama 56 waliochukua fomu katika jimbo la Mwanga wamerejesha 55, Moshi Vijijini waliochukua ni 47 na waliorejesha ni 46, Moshi Mjini waliochukua ni 37 na waliorejesha 34, Vunjo waliochukua ni 39 na waliorejesha ni 38.

Amesema, katika majimbo matano ambayo wanachama wake walichukua fomu na kuzirejesha zote ni Rombo walichukua 55, Hai 42, Siha 39, Same Magharibi 41 na Same Mashariki 36.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na CCM makao makuu kuhusu mchakato huo, tarehe 20 na 21 Julai ni mikutano mikuu ya majimbo na wilaya yenye lengo la kupiga kura za maoni kwa wabunge na wajumbe wa baraza la wawakilishi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!