Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Majaliwa ahimiza viongozi wa dini kuhubiri amani
Habari Mchanganyiko

Majaliwa ahimiza viongozi wa dini kuhubiri amani

Spread the love

WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewataka viongozi wa dini na Watanzania kwa ujumla watumie nyumba za ibada kuhubiri suala la amani na utulivu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Lindi…(endelea).

Taarifa iliyotumwa kwa umma na ofisi ya waziri mkuu imesema, Majaliwa ametoa wito huo leo Ijumaa tarehe 17 Julai 2020 wakati akizungumza na waumini wa dini ya Kiislamu alipohudhuria sala ya Ijumaa katika msikiti wa Buhari uliopo Ruangwa, mkoani Lindi.

Waziri mkuu amesema, ni muhimu Watanzania wakajenga tabia ya kuaminiana, kuvumiliana pamoja na kupendana kwani mambo haya yote huchangia uwepo wa amani na utulivu.

“Nchi hii imejizolea sifa kuwa ni nchi ya amani na utulivu kwa sababu jambo hili linahubiriwa na viongozi wa dini zote. Nchi hii sasa imekuwa ni kimbilio la nchi ambazo zimepoteza amani kwenye nchi zao, wanakuja hapa wanajifunza na wakirudi kwao wanaendelea kuwa salama,” amesema.

Majaliwa amesema, ni jukumu la kila Mtanzania kuzingatia mahubiri ya viongozi wa dini ili nchi iendelee kuwa na amani kwani kukiwa na amani na utulivu lazima maendeleo yataonekana.

“Nchi yetu imekuwa na kasi ya maendeleo katika maeneo mengi. Mimi naamini maendeleo haya yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na amani tuliyonayo na hii inatokana na mahubiri ya viongozi wetu wa dini. Dini ina mchango mkubwa sana katika uendeshaji wa Serikali,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!