Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Wapinzani waichongea CCM Takukuru
Habari za Siasa

Wapinzani waichongea CCM Takukuru

Benson Kigaila, Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)
Spread the love

WANASIASA wa vyama vya upinzani nchini Tanzania, wamekichongea Chama tawala cha Mapinduzi (CCM), katika Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Leo Ijumaa tarehe 17 Julai 2020, katika warsha ya wadau wa uchaguzi na Takukuru, iliyofanyika jijini Dar es Salaam, wanasiasa hao wameitaka Takukuru kufuatilia karibu mchakato wa uchaguzi ndani ya CCM kwa madai unaweza ukazungukwa na vitendo vya rushwa .

Warsha hiyo iliyolenga kujadili namna ya kudhibiti vitendo vya rushwa katika mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020, ilihudhuriwa na viongozi wa dini, vyama vya siasa na taasisi zinazosimamia siasa na uchaguzi.

Renatus Muabhi, Katibu Mkuu wa Chama Cha Kijamii (CCK), ameishauri Takukuru kukifuatilia kwa karibu CCM kwa madai kwamba kina uwezekano mkubwa wa kugubikwa na rushwa katika mchakato wake wa uchaguzi, kwa kuwa kina rasilimali fedha nyingi.

“Chama kikubwa ndio vinanyooshewa mikono, vina fedha. Tumesikia watu wa CCM Takukuru inavyoshughulika nayo. Vidogo havina tatizo sababu havina ushawishi wala rasilimali fedha,” amesema Muabhi.

Muabhi amesema, Takukuru imefanya vyema kuwaita wadau wa uchaguzi, kwa kuwa itapata mbinu nyingi haramu zinazotumiwa na wanasiasa kurubuni wananchi.

“Kuna mbinu nyingi ambazo taasisi inashindwa kubaini hili, wanasiasa wana mbinu nyingi na Takukuru imefanya vyema kutuita, wanataka tuwaeleze ghiliba mbalimbali zinazotumiwa na wanasiasa kupata kura kupitia rushwa,” amesema Muabhi.

Renatus Muabhi, Katibu wa Chama cha CCK.

Benson Kigaila, Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), akizungumza katika mjadala huo, amehoji tafsiri ya wafungwa kupandisha bendera za CCM, kama ni rushwa au sio rushwa.

Katika maandalizi ya mkutano wake mkuu wa CCM uliofanyika kuanzia tarehe 10 hadi 11 Julai 2020, kuna picha zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii, zikionesha baadhi ya wafungwa wakipandisha bendera za CCM jijini Dodoma.

Kigaila amedai, kitendo hicho hakileti usawa kwa vyama vya siasa vya upinzani na kudai kwamba hakina tofauti na rushwa.

“Hali ninayoiona bado tunaingalia rushwa kwa jicho moja. Rushwa maana yake ni matumizi mabaya ya madaraka, mtu aliyopewa kupata masilahi binafsi.”

“Halijachukulia kama suala pana kiasi hicho. Unafikiria ile suala la kutoa na kupokea rushwa. Mkurugenzi wa Takukuru anasema kuwe na usawa kwenye uchaguzi, vitendo vinavyofanyika kutoleta usawa ni rushwa,” amedai Kigaila.

Kigaila ameipongeza Takukuru kwa kuandaa warsha hiyo, kwa kuwa wadau wa siasa watapa fursa ya kuhoji mambo yenye viashiria vya rushwa.

“Mfano Jeshi la Magereza kupandisha bendera za chama, wengine hawawezi hiyo ni rushwa lazima ipingwe. Ni vizuri tutatumia huu muda (warsha), kueleza sio vizuri na tutafanyaje kuzuia hilo,” amesema Kigaila

Kigaila amedai, “wao wanashughulika na kutoa rushwa lakini matumizi ya madaraka kuwa ni rushwa hawaoni, rushwa sio kupokea hela, ni kumnyima mtu kutokuwa sawa na mazingira ya uchaguzi kutokuwa sawa hio ni rushwa.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

error: Content is protected !!