Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko CCM haijatimiza ahadi ya uvuvi – Zitto
Habari Mchanganyiko

CCM haijatimiza ahadi ya uvuvi – Zitto

Zitto Kabwe, Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalando
Spread the love

ZITTO Kabwe, Kiongozi Chama cha ACT-Wazalendo, amewataka wananchi kutoipa kura CCM kwa kuwa, imeshindwa kutimiza ahadi zake za mwaka 2015. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam…(endelea)
Kauli hiyo aliitoa Zitto wakati akiwa kwenye ziara yake, Kigoma mbele ya wanachama wa chama hicho kwenye Jimbo la Kigoma Kusini.

Akizungumza na wanachama hao, Zitto amehoji, kwanini vyombo vya uvuvi baharini viwe na leseni ikiwa havina tofauti ya utendaji kazi wake na Trekta linalotumiwa kwa ajili ya kilimo?.

“Mkulima nyenzo yake ya kumwezesha kufanya kilimo ni Trekta ambalo Mamlaka ya Usafari wa Majini na Ardhini (Sumatra), hawatoi lesini kwa ajili ya chombo hicho ili kilime, kwanini chombo kinachotumika na wavuvi kuvulia (Kipe) Sumatra wanatoa lesini kwa ajili ya kukiendesha chombo hicho ilhali wote wanafanya kazi zinazofanana?” amehoji Zitto na kuongeza:

Zitto amesema, CCM imeahidi mambo 16 kuwafanyia wavuvi ikiwemo uvuvi wa baharini na ule wa maji ya baridi, na kwamba

“hakuna ahadi hata moja waliyoitekeza ya uvuvi hadi miaka mitano imeisha.”

Ametaja miongoni mwa ahadi hizo ni pamoja na Meli kubwa tano za uvuvi ambazo zitazalisha ajira za watu elfu 15.

“Waliahidi kwamba, watafungua bandari ya uvuvi kule Pwani lakini miaka mitano imekatika, hawajafungua bandari hiyo,” amesema.

Zitto ambaye alikuwa Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini amesema, Serikali ya CCM imewatia umasikini wavuvi kwa kuwachomea moto nyavu zao.

“Mwaka 2014 thamani ya mauzo ya bidhaa za uvuvi zilifikia Dola za Marekani kama milioni 832, mwaka huu mauzo yameshuka mpaka Dola milioni 158, sisi chama chetu kinakwenda kupigania kwamba kama mkulima hana leseni kwenye trekta, na mvuvi asiwe na leseni kwenye chombo,” amesema Zitto.

Amesema, chama hicho kitapunguza leseni za uvuvi na kwamba kutakuwa na leseni moja ya utambuzi wa chombo yenye gharama ndogo.

Awali, Sendwe Ibrahim, Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo Mkoa wa Kigoma amesema, faini ya chombo cha uvuvi ina thamani sawa na bei ya chombo chenyewe.

“Faini ya chombo ni sawa na Shilingi  milioni tatu ambayo ni sawa na thamani ya chombo, Ziwa Tanganyika tunapakana na Congo,  Burundi na Zambia, sheria zinazotumika Tanzania, Kongo, Burundi na Zambia hakuna sheria hizi, tumetungiwa sisi ilhali samaki hawajui mipaka,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!