October 2, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mwandishi wa habari ajitosa ubunge Iringa

Spread the love

MWANDISHI wa habari nchini Tanzania, Tumain Msowoya amechukua fomu ya kuwania ubunge viti maalum kupitia Umoja wa Wanawake Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (UWT) Mkoa wa Iringa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Iringa…(endelea)

Tumain amekabidhiwa fomu hizo leo Jumanne tarehe 14 Julai 2020 na Katibu wa UWT Mkoa wa Iringa, Angela Milembe katika Ofisi za CCM mkoani humo.

Mwandishi huyo wa habari amewahi kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM) Mkoa wa Iringa.

Baada ya kumkabidhi fomu, MIlembe ametoa wito kwa wanawake kujitokeza kuchukua fomu kwani bado zipo.

Tumain ambaye kwa sasa ni Afisa Habari wa Kampuni ya  kuzalisha nguzo za umeme ya Qwihaya amewahi kutunukiwa tuzo ya heshima ya udaktari kutoka Chuo Kikuu cha The African Graduate cha nchini Sierra Leone

Alitunukiwa kutokana na kazi za uandishi wa habari hasa zilizohusisha masuala ya wanawake, watoto na watu wenye ulemavu.

error: Content is protected !!