Monday , 6 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa IGP Sirro: Kama Mbowe kadanganya…
Habari za Siasa

IGP Sirro: Kama Mbowe kadanganya…

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema
Spread the love

SIMON Sirro, Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP) amesema, kama Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kadanganya kuhusu kushambuliwa kwake, atafikishwa mahakamani. Anaripoti Hamis Mguta, Dar es Salaam…(endelea).

Akizungumza na ITV katika kipindi cha Dakika 45 amesema, Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi kuhusu tukio la kushambuliwa Mbowe lililotokea usiku wa kuamkia tarehe 9 Juni 2020.

Mboye ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni alikutwa na kadhia hiyo, wakati akirejea katika makazi yake yaliyopo eneo la Area D, jijini Dodoma.

Katika mahojiano hayo, IGP Sirro amesema, tukio la Mbowe bado lipo kwenye uchunguzi ili kubaini taarifa alizozitoa zina uhalisi ama la na kwamba kama ni halisi, nani aliyehusika.

IGP Simon Sirro

“Siku zote shahidi namba moja ni kwenye eneo la tukio. Sasa kama eneo la tukio ushahidi hakuna na kila mtu anasema hajasikia… hajasikia…hajasikia! Sitaki nimuhukumu mtu, lakini upelelezi unaendelea,” amesema

“Ila ninataka Watanzania waelewe kwamba, tukibaini kuna taarifa ya uongo, ninarudia, tukibaini kuna tarifa ya uongo, hakuna mtu aliye juu ya sheria, tutampeleka mahakamani kwa kutoa taarifa ya uongo,” alisisitiza.

Kwenye mazungumzo hayo, IGP Sirro alisema, walilazimika kutumia nguvu ya ziada kumuhoji dereva wa Mbowe ili aseme chochote.

Alidai, dereva huyo alizuiwa kusema.

Alisisitiza, mtu anayetoa taarifa za kushambuliwa ni lazima wafanye uchunguzi ikiwa ni pamoja na kutaka kujua kama je, ameshambuliwa? “ni lazima tufanye hivyo kwa sababu si kila taarifa huwa ni sahihi.”

Baada ya tukio la kushambuliwa kwa Mbowe, alipelekwa Hospitali ya DCMC Ntyuka

Dodoma na siku hiyohiyo jioni alihamishiwa Hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam kwa matibabu zaidi.

Kwa sasa, Mbowe anaendelea na matibabu akiwa nyumbani kwake Dar es Salaam huku akitumia magongo kutembea kutokana na kuumia mguu wa kulia katika tukio hilo lililomtokea.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali kutafuta mwekezaji mwingine Bandari ya Dar es Salaam

Spread the loveSERIKALI inaendelea kutafuta mwekezaji mwingine atakayeendesha gati namba nane hadi...

Habari za SiasaTangulizi

Kinana: Hatukubali kushutumiwa kwa uongo

Spread the loveMakamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Abdulrahman Kinana amesema viongozi wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mbatia ambwaga Selasini, mahakama yaamuru alipwe fidia

Spread the loveMAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imemuamuru...

Habari za SiasaTangulizi

Mkulo afariki dunia, kuzikwa kesho Kilosa

Spread the loveALIYEKUWA Waziri wa Fedha na Mbunge wa Kilosa (CCM), Mustafa...

error: Content is protected !!