Tuesday , 7 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Kampeni 2020: Facebook yang’oa matangazo ya Trump
Kimataifa

Kampeni 2020: Facebook yang’oa matangazo ya Trump

Spread the love

MTANDAO wa kijamii wa Facebook, umeng’oa matangazo ya kampeni ya Donald Trump, Rais wa Marekani kwamba yanachochea ubaguzi. Inaripoti mitandao ya kimataifa…(endelea).

Taarifa ya mtandao huo imeeleza, imechukua hatua hizo kwa haraka kwa kuwa, alama anazotumia Trump kwenye matangazo yake ndizo zilizokuwa zikitumiwa na utawala wa Kinazi wa Ujerumani.

Kampuni hiyo imetolea mfano tangazo lenye alama ya pembe tatu nyekundu, ambapo alama hiyo na tangazo hilo hilo lilitumika na utawala wa kinazi kuwatambua wapinzani wao kama wakomunisti.

Hata hivyo, timu ya kampeni ya Trump imelalamika hatua iliyochukuliwa na Facebook kwamba, alama ama tangazo hilo, halikulenga ubaguzi bali likilenga kikundi cha wanaharakati wa mrengo wa kushoto Antifa.

Sababu ya mtandao huo kuchukua uamuzi huo ni kwamba, ubaguzi wa aina yoyote ikiwemo chuki, ni sera inayipingana na matakwa ya kampuni hiyo.

 

“Haturuhusu alama ambazo zina simama kwa mirengo ama makundi ya chuki, labda iwe ni kukemea jambo hilo,” ameeleza mkuu wa sera za ulinzi wa Facebook, Nathaniel Gleicher na kuongeza:

“Hiko ndicho tulichokiona kwenye tangazo hili, na popote pale alama hiyo itakapotumika tutachukua hatua kama hii.”

Matangazo hayo yalipachikwa kwenye ukurasa wa Trump na Mike Pence, makamu wake ambapo yamedumu kwenye kurasa hizo kwa saa 24.

“Pembe tatu nyekundu ni alama inayotumiwa na antifa, hivyo ilitumika katika tangazo kuhusu antifa.”

“Tunatambua kama Facebook wana kibonzo (emoji) cha pembe tatu nyekundu, pia ambacho ni sawa kabisa ile tuliyotumia,” ameeleza Tim Murtaugh, msemaji wa timu ya kampeni ya Trump.

Hata hivyo, Trump ameelekeza shutuma zake kwa la antifa kwamba limekuwa likichochea maandamano na vurugu kote nchini Marekani, kutokana na kifo cha George Floyd, mmarekani mweusi kilichotokea mikononi mwa polisi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Israel yatia shubiri Gaza wakisherehekea Hamas kusitisha mapigano

Spread the loveWAKATI kundi la Hamas huko Gaza likitangaza kuridhia pendekezo lao...

KimataifaMakala & Uchambuzi

Mbivu, mbichi urais wa Ramaphosa mwezi huu

Spread the loveMWISHONI mwa mwezi huu, raia wa Afrika Kusini watapiga kura...

Habari za SiasaKimataifa

Mwanamke Rwanda ataka kupambana tena na Kagame

Spread the loveKIONGOZI wa kihistoria wa upinzani nchini Rwanda, Victoire Ingabire Umuhoza,...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

error: Content is protected !!