Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Spika Ndugai awachongea wabunge kwa wananchi, avikosoa vyombo vya habari
Habari za Siasa

Spika Ndugai awachongea wabunge kwa wananchi, avikosoa vyombo vya habari

Spika wa Bunge, Job Ndugai
Spread the love

SPIKA wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai ameshauri wananchi kutowachagua wabunge walopokaji na watovu wa nidhamu. Anaripoti Mwandishi Wetu. …(endelea).

Spika Ndugai ametoa wito huo leo Ijumaa tarehe 19 Juni 2020, wakati akihojiwa na Clouds TV, kuhusu  changamoto zilizojitokeza katika shughuli za Bunge la 11, lililovunjwa na Rais John Magufuli, tarehe 16 Juni 2020.

Amesema, katika Bunge lake, vitendo vya utovu wa nidhamu vilikithiri huku akituhumu vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, kuchochea vitendo hivyo kwa kuwapa vipaumbele wabunge walopokaji.

Spika Ndugai amedai, baada ya wabunge wanaofanya makosa kuadhibiwa, vyombo vya habari huwabeba kwa kutoa taarifa zao.

“Tulisema mwaka mzima itakuwa adhabu kubwa lakini hata akienda huko (mbunge ) anatamba ni shida sana na watu kama hawa wanaonekana kwa vijana kama mashujaa. Vyombo vya habari na mitandao inakuza watu wa ovyo. Wasema ovyo na walopokaji wanafanywa kuwa mashujaa,” amesema Spika Ndugai.

Spika Ndugai amesema, changamoto hiyo inatakiwa itafutiwe ufumbuzi ili isijitokeze tena katika Bunge la 12 linalotarajiwa kuanza tena Novemba 2020.

Spika Ndugai amesema, ili changamoto hiyo imalizike, inatakiwa wananchi wasiwarudishe bungeni, wabunge wenye tabia hizo, pamoja na vyombo vya habari kuacha kutoa taarifa zao.

“Kuendeela kurusha taarifa za wabunge hao si sawa, ndio maana tunahitaji msaada wa vyombo vya habari tunapoelekea Bunge la 12,  kuona Bunge la 12 tufanyaje kutatua hili tatizo,“ amesema Spika Ndugai

“Bahati nzuri naamini wapiga kura watachuja, sababu waliowengi katika hawa sababu ukiacha ulopokaji wao bungeni,  hakuna walichofanya bungeni wao ni kulopoka na kulaumu,  lakini hakuna cha maendeleo walichofanya majimboni kwao,” amesema Spika Ndugai pasina kuwataja kwa majina

Spika Ndugai amesema, kukithiri kwa vitendo vya utovu wa nidhamu katika bunge hilo, kulisababisha mikutano yake kutorushwa mubashara kama ilivyokuwa katika mikutano ya mabunge yaliyopita.

Amedai kuwa, wabunge wengi wakiona kamera wanabadilika na kuonyesha tabia mbaya, lakini kamera zikiwa hazipo wanafikiri sawasawa.

“Tukafika mahali ambapo ‘live Camera’ ikaliharibu bunge, watu wakawa wanatukana, wanatabia mbaya, unakuta mmekubaliana kwenye kanuni kuwe na nidhamu lakini watu wanabadilika wanacheza mchezo wa kuigiza, “ amesema Spika Ndugai

“Wanacheza na wananchi kupotosha kila kitu, tukagundua kwa nini mtu kamera ikiwa haipo anafikiri sawasawa,  ikiwa ipo anabadilika, ni moja ya sababu ikapeleka tuangalie nini la kufanya.”

Hata hivyo, sababu ambazo zilitolewa wakati Nape Nnauye, aliyekuwa waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo akitoa sababu za kusitisha matangazo ya moja kwa moja ya Bunge ‘Bunge Live’ alisema ni suala la gharama kuwa kubwa.

Pia, alisema, kitendo cha Bunge kuonyeshwa ‘live’ kiliwafanya wananchi kutokufanya kazi na kubaki wakifuatilia Bunge.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!