Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbunge: Wageni hawaingii Tanzania kuhofia usalama wao
Habari za Siasa

Mbunge: Wageni hawaingii Tanzania kuhofia usalama wao

Frank Mwakajoka, Mbunge wa Tunduma
Spread the love

MBUNGE wa Tunduma, Frank Mwakajoka (Chadema) amesema, Serikali imeshindwa kutatua tatizo la upatikanaji wa umeme katika mpaka wa Tunduma mkoani Songwe kwa muda mrefu jambo linalosababisha kupoteza wageni na wateja wa bandari ya Dar es Salaam kwa kuhofia usalama wao kutokana na giza. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Kutokana na hali hiyo, Mwakajoka ameihoji  Serikali na kutaka kujua kama iko tayari kuunganisha umeme wa Zambia ili huduma ya nishati ya umeme iwe inapatikana muda wote ikiwa ni kulinda wateja wanaopitisha mizigo toka bandari ya Dar es Salaam na mpaka wa Tunduma.

Wizara ya Nishati ikijibu swali hilo ilisema, Mji wa Tunduma unatumia umeme wa Gridi ya Taifa kwa asilimia 100 kupitia njia ya msongo wa kilovoti 33 kutoka Kituo cha kupoza Umeme cha Iyunga, Mjini Mbeya na kusambaza umeme katika maeneo ya Wilaya za Mbozi, Momba na Songwe.

Imesema kwa ujumla, hali ya upatikanaji umeme kwa sasa ni ya kuridhisha, hata hivyo, hitilafu katika baadhi ya miundombinu ya umeme imekuwa ikisababisha kuzima umeme ili kupisha matengenezo katika njia kuu ya umeme katika Mkoa wa Songwe na baadhi ya maeneo ya Wilaya ya Mbeya vijijini.

Katika majibu hayo, wizara hiyo imesema, Serikali kupitia TANESCO imekarabati miundombinu ya umeme ili kuimarisha upatikanaji wa umeme katika maeneo hayo.

“Aidha, katika mwaka wa fedha 2020/21 TANESCO imepanga kujenga kituo cha umeme Mlowo (switching station) pamoja na njia ya umeme msongo wa kilovoti 33 yenye urefu wa kilomita 65 kutoka kituo cha kupoza umeme cha Iyunga Mbeya hadi Mlowo kwa gharama ya Shilingi Bilioni 1.2.

“Mradi huu unatarajia kuanza kutekelezwa Mwezi Julai, 2020 na kukamilika Mwezi Mei, 2021 kupitia Kampuni ya TANESCO M/S Electrical Transmission and Maintenance Company (ETDCO) Limited,” imesema

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!