Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Dk. Lwaitama: Ni uhuru wa mawazo wa wabunge Chadema
Habari za Siasa

Dk. Lwaitama: Ni uhuru wa mawazo wa wabunge Chadema

DK. Azaveli Lwaitama, Mhadhiri mstaafu
Spread the love

HATUA ya baadhi ya wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kupuuza uamuzi wa chama hicho wa kutoendelea na vikao vya Bunge, imeelezwa kuwa si tatizo bali uhuru wa mawazo. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).

Dk. Azaveli Lwaitama, Mhadhiri Mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akizungumza na akizungumza na MwanaHALISI Online leo tarehe 5 Mei 2020, kuhusu wabunge hao kuhudhuria vikao vya bunge kinyume na mzimamo wa chama hicho, amesema “kila mmoja ana uhuru wake, na wala sio tatizo.”

Amesema, ndani ya chama cha siasa hasa chenye misingi ya kidemokrasia, lazima utofauti na mikinzano iwepo na kwamba ndio afya ya demokrasia.

“Kutofautiana sio tatizo, kwa sababu ndio misingi ya chama chenyewe. Katika kundi la watu wengi, ni uhuru wao wa kuwaza tofauti,” amesema Dk. Lwaitama.

Miongoni mwa wabunge waliokaidi agizo hilo ni Joseph Selasini (Rombo), Anthony Komu, (Moshi Vijijini) na David Silinde (Momba) ambaye alikuwa Katibu wa Wabunge wa Chadema.

Wengine ni Peter Lijualikali (Kilombero), Jafary Michael (Moshi Mjini) na wabunge viti maalumu, Ratifa Chande, Mariam Msabaha, na Sabrina Sungura.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!