Tuesday , 7 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Virusi vya corona: Mbio za Mwenge zasitishwa 
Habari Mchanganyiko

Virusi vya corona: Mbio za Mwenge zasitishwa 

Spread the love

RAIS John Magufuli amesitisha mbio za Mwenge na kuagiza fedha zilizotengwa kwa ajili ya kufanikisha zoezi hilo iende Wizara ya Afya kwa ajili ya kununua vifaa na dawa za kudhibiti  janga la mlipuko wa virusi vya Corona. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo tarehe 16 Machi 2020, alipofanya ziara ya kushtukiza ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara za juu Ubungo, jijini Dar es Salaam.

“ Mbio za Mwenge hazitafanyika mpaka tuhakikishe Corona imeisha,” ameagiza Rais Magufuli.

Ugonjwa wa COVID-19 unaosababishwa na mlipuko wa virusi hivyo, unasambaa kwa kasi ulimwenguni, ambapo kwa sasa umeanza kutikisa barani Afrika.

Katika ukanda wa Afrika Mashariki, nchi ya Kenya, Rwanda zimeripoti kuwa na waathirika wa ugonjwa huo. Ambapo zimepiga marufuku mikusanyiko ya watu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mahakama yatoa uamuzi zuio dhidi ya Club House

Spread the loveMAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu jijini Dar es Salaam,...

Habari Mchanganyiko

GGML, OSHA yawanoa bodaboda 200 Arusha

Spread the loveZAIDI ya madereva bodaboda 200 wa jiji la Arusha wamepatiwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Serikali kuwakopesha wajasiriamali 18.5bn/- kupitia NMB

Spread the loveSerikali imetenga kiasi cha Sh 18.5 bilioni kwa ajili ya...

AfyaHabari Mchanganyiko

Huduma za kibingwa zazinduliwa katika hospitali za halmashauri 184

Spread the loveSERIKALI imezindua huduma za matibabu za kibingwa katika hospitali 184...

error: Content is protected !!