RAIS John Magufuli amesitisha mbio za Mwenge na kuagiza fedha zilizotengwa kwa ajili ya kufanikisha zoezi hilo iende Wizara ya Afya kwa ajili ya kununua vifaa na dawa za kudhibiti janga la mlipuko wa virusi vya Corona. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).
Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo tarehe 16 Machi 2020, alipofanya ziara ya kushtukiza ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara za juu Ubungo, jijini Dar es Salaam.
“ Mbio za Mwenge hazitafanyika mpaka tuhakikishe Corona imeisha,” ameagiza Rais Magufuli.
Ugonjwa wa COVID-19 unaosababishwa na mlipuko wa virusi hivyo, unasambaa kwa kasi ulimwenguni, ambapo kwa sasa umeanza kutikisa barani Afrika.
Katika ukanda wa Afrika Mashariki, nchi ya Kenya, Rwanda zimeripoti kuwa na waathirika wa ugonjwa huo. Ambapo zimepiga marufuku mikusanyiko ya watu.
Leave a comment