Monday , 6 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Zitto ‘kupigwa chini’ ACT-Wazalendo?
Habari za SiasaTangulizi

Zitto ‘kupigwa chini’ ACT-Wazalendo?

Spread the love

ISMAIL Jussa, Mwenyekiti wa Kamati ya Mikakati, Usimamizi na Ufuatiliaji ya Chama cha ACT-Wazalendo, anataka nafasi aliyonayo Zitto Kabwe. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Kwa sasa Zitto ni Kiongozi Mkuu wa chama hicho, ambapo Jussa amechukua fomu tarehe 25 Februari 2020 kumkabili Zitto kwenye nafasi hiyo.

Chama hicho kinatarajia kufanya uchaguzi wa viongozi wakuu tarehe 14 Machi 2020, baada ya kukamilika kwa uchaguzi wa ngome za wanawake, vijana na wazee.

Jussa anakuwa manachama wa tatu kuomba nafasi hiyo, waliomtangulia ni Zitto mwenyewe ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Mjini na Joseph Mona, Katibu wa ACT-Wazalendo Mkoa wa Katavi.

Nafasi hiyo kwa sasa inashikiliwa na Mbunge wa Kigoma Mjini na mmoja wa waasisi wa chama hicho, Zitto Kabwe.

Jussa ambaye alijiunga na chama hicho mwaka jana akitokea Chama cha Wananchi (CUF), anakuwa mwanachama wa tatu kuchukua fomu kuwania nafasi hiyo.

Nafasi alizowahi kutumikia Jussa

Jusa (48), aliwahi kuwa Mbunge wa kuteuliwa katika Bunge la Jamhuri, aliteuliwa na Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete, aliwahi kuwa mwakilishi katika Bunge la Wawikilishi Zanzibar pia aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa CUF.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Jacob, Malisa wapandishwa kizimbani kwa mashtaka ya uongo mitandaoni

Spread the loveMKURUGENZI wa Shirika la Haki, Godlisten Malisa na mwanachama wa...

BiasharaHabari za Siasa

Bunge laitaka Serikali kudhibiti ufisadi miradi ya mkakati

Spread the loveKAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, imeitaka Serikali kuimarisha...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Wizara ya Uchukuzi yaomba kuongezewa bajeti na Bunge

Spread the loveWIZARA ya Uchukuzi imeliomba Bunge liidhinishe bajeti yake kwa mwaka...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali kutafuta mwekezaji mwingine Bandari ya Dar es Salaam

Spread the loveSERIKALI inaendelea kutafuta mwekezaji mwingine atakayeendesha gati namba nane hadi...

error: Content is protected !!