Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Zitto alianzisha Kigoma, wenyeviti CCM ‘walia njaa’
Habari za SiasaTangulizi

Zitto alianzisha Kigoma, wenyeviti CCM ‘walia njaa’

Spread the love

WAJUMBE wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji, wamegoma kuwatambua wenyeviti wa serikali za mitaa waliopita bila kupingwa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kigoma … (endelea).

Wajumbe wa baraza hilo wameazimia wenyeviti hao wasilipwe posho, kwa madai kwamba sio viongozi halali, kwa kuwa hawakuchaguliwa na wananchi.

Azimio hilo limepitishwa kikao cha Baraza la Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji, lililokutana katika kikao chake cha kwanza kwa mwaka 2020.

Uamuzi huo umefikiwa baada ya Obadia Andrea Manwingi, Diwani wa Katubuka kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuhoji kwamba lini halmashauri hiyo itapeleka posho hizo kwa wenyeviti wa serikali za mitaa, vitongoji na vijiji.

Baada ya hoja hiyo, Zitto Kabwe, Mbunge wa Kigoma Mjini aliwataka wajumbe wa baraza hilo, kuweka azimio la kushinikiza halmashauri hiyo isitoe posho kwa wenyeviti, kwa madai kwamba fedha za walipa kodi haziwezi kutumiwa na viongozi wasio na ridhaa ya wananchi.

“Mheshimiwa Diwani, naomba usahau kuhusu malipo ya posho kwa wenyeviti hawa waliowekwa bila ridhaa ya wananchi, mpaka baraza hili linamaliza muda wake. Hatuwezi kutumia kodi za wananchi kuwalipa wenyeviti haramu, wasitegemee ushirikiano wowote na baraza hili ,” amesema Zitto.

“ACT Wazalendo inatoa wito kwa wananchi na vyama makini vya upinzani, vinavyoongoza halmashauri kutowatambua wenyeviti hawa haramu na kutowapa ushirikiano wowote kiutendaji.”

Kikao hicho kiliongozwa na Mstahiki Meya Hussein Ruhava. Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji ina Kata 19 Mitaa 68 na Madiwani 18 ACT Wazalendo, 7 CCM  na 1 CHADEMA.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Sauti ya Watanzania waeleza sababu za kuiunga mkono Chadema

Spread the love  KIKUNDI kinachojipambanua katika kupigania rasilimali na uhuru wa nchi,...

Habari MchanganyikoTangulizi

Jacob, Malisa waachiwa kwa masharti

Spread the love  JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

error: Content is protected !!