April 14, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Kauli ya matumaini usajili laini za simu

Spread the love

WANANCHI ambao hawajasajili laini zao za simu, lakini tayari wamefanya baadhi ya taratibu, busara itatumika. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kogoma … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa na Atashasta Nditiye, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano mkoani Kigoma.

Amesema, wananchi ambao taarifa zao zipo kwenye Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), na hawajapata vitambulisho au namba kwa sababu mbalimbali, serikali itaona namna ya kufanya kuhakikisha wanaendelea kupata huduma “lakini wale ambao hawajajaza fomu kusajili, laini zao zitazimwa.”

Ameeleza kuwa, zoezi la usajili wa laini halitaisha tarehe 20 Januari 2020 kama ilivyotangazwa, na kwamba zoezi hilo ni endelevu.

error: Content is protected !!