October 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Zitto ashtukia “wananitafuta wanifungulie kesi”

Spread the love

ZITTO Kabwe Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo ameeleza kuwa zipo njama zinazofanywa dhidi yake ili akamatwe na kushtakiwa kwa kesi ya utakashaji fedha kwa lengo la kumfanya akose kushiiriki uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020, Anaripoti Mwandishi wetu, Kigoma … (endelea).

Akizungumza na wafuasi wa chama hicho mkoani Kigoma amesema kuwa anatafutwa kwa dhamira ya kutengezewa kesi ya utakatishaji fedha ambayo haina dhamana ila asishiriki uchaguzi Mkuu wa kumchagua Madiwani, Wabunge na Rais.

“Mimi najua wananitafuta sasa hivi wanitengezee kesi ya utakatishaji fedha ili waniweke ndani uchaguzi unikute niko ndani…” amesema Zitto.

Amesema kuwa njama za awali ni kumzuia asichukue fomu ya kugombea nafasi anayokusudia lakini wameona hawataweza wakaona wabadilishe namna.

“Wameamua ama wazuie nisichukue fomu au waniweke ndani, wameona bora waniweke ndani hivi sasa viongozi wetu, madiwani wetu wameitwa Takukuru leo, karibu viongo wetu wote wameitwa Takukuru.

“Kuna diwani mmoja wa Mwandiga alikuwa Mwenyekiti wa serikali ya kijiji zamani wakati ule ndio nimekuwa Mbunge  nikawa nataka nijenge nyumba nikaomba kiwanja kwenye Serikali ya kijiji, wakamuandikia barua kwamba tuletee maombi yote aliyofanya Zitto ya kuomba viwanja na ardhi eti wanachunguza taarifa zangu zote. Nimeweka wazi  na miaka yote naweka wazi hamna kitu kipya watakachokutana nacho…” amesema Zitto.

Amesema kuwa wanaweza kumtengenezea shauri hilo kwa kuwa tayari wamekusudia  “wanaweza kutengeza mashtaka yoyote na wala mkisikia msishangae kwa sababu hawana namna ya kushinda na sisi kwa hoja,” amesema Zitto.

error: Content is protected !!