Sunday , 5 May 2024
Home Kitengo Michezo Simba vs Yanga maandalizi yakamilika, vingilio vyatajwa
Michezo

Simba vs Yanga maandalizi yakamilika, vingilio vyatajwa

Spread the love

Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) sambamba na bodi ya ligi wamekamilisha maandalizi yote kuelekea mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakao wakutanisha miamba miwili ya soka nchini Simba dhidi ya Yanga, ikiwemo kutoa majina ya waamuzi watakao chezesha mchezo huo sambamba na kutaja viingilio kwenye mchezo huo. Anaripoti Kelvin Mwaipungu… (endelea)

Makamu M/nyekiti wa bodi ya ligi Ibrahim Mwayelwa ameeleza kuwa mchezo huo ni mkubwa sana kwenye historia ya mpira wa Tanzani kwa kuwa unakusanya idadi kubwa ya mashabiki hivyo wameshaimalisha maswala  mbali mbali ikiwamo ulinzi na namna mashabiki watakavyoweza kuingia uwanjani bila usumbufu wowote.

“Asilimia kubwa ya maandalizi yamesha kamilika ikiwamo kutaja waamuzi wa mchezo huo na bado vikao mbalimbali vinafanyika ili kuufanya mchezo huu kuchezwa kwa taratibu na kanuni zinazohitajika ili uweze kumalizika salama” alisema Ibrahim Mwayelwa

Mwayelwa aliongezea kuwa mpaka sasa tiketi za mchezo huo zimesha anza kuuzwa kwa mawakala wote wa Selcom hivyo ametaka mashabiki kununua mapema ili kuepuka usumbufu ambapo tiketi za VIP A zitauzwa kwa shilingi 30000, VIP B na C zitakuwa shilingi 20000 huku mzunguko zitauzwa kwa bei ya shilingi 7000.

Mwamuzi wa kati wa mchezo huo atakuwa Jonesian Rukya (Kagera) huku akisaidiwa na Hamisi Chang’walu na Sudi Lila pamoja na mwamuzi wa akiba Elly Sasii wote kutoka (Dar es Salaam) huku kamishna wa mchezo ni Khalid Bitebo kutoka Mwanza.

Mchezso huo unatarajian kuanza majira ya saa 11 jioni kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam huku timu zote zikisaka ushindi kujiweka sehemu nzuri kwenye msimamo wa ligi.

Mara ya mwisho zilipokutana timu hizi mbili Yanga ilipoteza mchezo huo kwa kukubali kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Simba, bao lilifungwa na mshambuliaji Meddy Kagere kwa njia ya Kichwa akipokea pasi kutoka kwa Johhn Bocco.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Usiishie kuangalia tu game za leo, piga na mkwanja na Meridianbet

Spread the love  LIGI mbalimbali barani ulaya zitarejea tena Jumamosi ya leo...

Michezo

Ligi mbalimbali za pesa kuendelea leo

Spread the love Ijumaa ya leo ambapo mechi mbalimbali zinaendelea Duniani Meridianbet...

Michezo

Europa na Conference kukupatia pesa ndefu leo

Spread the love  ALHAMISI ya leo tutaenda kushuhudia mitanange ya kukata na...

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

error: Content is protected !!