Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Mawakili binafsi wapigwa ‘stop’ NIDA
Habari Mchanganyiko

Mawakili binafsi wapigwa ‘stop’ NIDA

Spread the love

SERIKALI imepiga marufuku mawakili binafsi kutoa hati za viapo, kwa wananchi wanaosajili ili kupata Kitambulisho cha Taifa, kinachotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA). Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).

Agizo hilo amelitoa Mhandisi Hamad Masauni, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, baada ya kubaini upigaji unaofanywa na mawakili hao.

Mhandisi Masauni ameeleza kuwa, huduma zinazotolewa na mawakili hao zinatia shaka, huku akituhumu kwamba ni mradi wa baadhi ya maafisa wa NIDA na Idara ya Uhamiaji.

Amesema, baadhi ya watumishi wa NIDA na Uhamiaji huwaelekeza wananchi wanaotaka hati za kiapo, kwenda kwa mawakili hao, ambao hukaa pembezoni mwa ofisi zao.

“Inatia mashaka,  isije kuwa mradi wa watu wachache wasio waaminifu,  ole wao tukiwagundua. Kuanzia sasa ni marufuku kwa wananchi kwenda kulipa kule ili kupata huduma za wanasheria, kwanza hatujui namna juu ya utoaji wa hati hizo, kama zinatolewa kwa watu sahihi ama sio sahihi,” amesema Masauni na kuongeza;

“Lakini pili, huduma hizo ni kuwabebesha mzigo wananchi masiki, tatu kufunga mianya ya mahusiano kati ya watendaji wetu na wanasheria wanaotaka kujipatia fedha. Hivyo, kuanzia leo marufuku maafisa wa uhamiaji na NIDA kuelekeza watu kwenda kwa hao wanasheria.”

Mhandisi Masauni amesema, serikali itapeleka mawakili wake katika vituo vya NIDA, ili kuhakikisha wananchi wasiokuwa na uwezo wanaipata huduma hiyo.

“Wananchi hawa wengine hali zao ni za chini, wengine wanapata shida kupata fedha ya kupata chakula na familia zao. Sasa  unapomwambia kirahisi rahisi tu alipe 10,000 kwa ajili ya hati ya kipo ambayo haihakikiwi.

Na kibaya  zaidi nimepokea malalamiko ya watu zaidi ya wanne hapa, kwamba wanarudishwa, anakuja mara ya kwanza anaambiwa hati imepotea, anaelekezwa nenda pale nje utamuona mwanasheria,” amesema Mhandisi Masauni.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

error: Content is protected !!