Wednesday , 8 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Ikiwa zimebaki siku 10, TCRA yaonya wasiosajili alama za vidole
Habari Mchanganyiko

Ikiwa zimebaki siku 10, TCRA yaonya wasiosajili alama za vidole

Spread the love

IKIWA zimesalia siku kumi kwa watumiaji wasiosajili laini zao za simu kwa mfumo wa alama za vidole, kukatiwa mawasiliano, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imetahadharisha wahusika kwamba, msimamo huo hautabadilika. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Leo tarehe 21 Desemba 2019  kupitia ukurasa wake Twitter, TCRA imesisitiza ya kwamba mwisho wa matumizi ya laini zisizosajilwa ni tarehe 31 Desemba 2019, na hakutakuwa na muda wa nyongeza.

Mamlaka hiyo imewataka wananchi kuepuka usumbufu wa kukatiwa mawasiliano, kwa kujisajili mapema.

“Mwisho wa kutumia laini za simu ambazo hazijasajiliwa kwa kutumia namba ya kitambulisho cha Taifa na kuthibitisha kwa alama za vidole ni Desemba 31, 2019. Epuka usumbufu wa kukosa mawasiliano, sajili laini yako sasa,” imesisitiza taarifa ya TCRA.

Aidha, Mamlaka hiyo imewahimiza wananchi wasiokuwa na namba ya Kitambulisho cha Taifa, inayotolewa na Mamalaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), kufuata taratibu husika ili kupata namba hiyo, itakayowawezesha kusajili laini zao.

“Kama una laini ya simu lakini huna namba ya kitambulisho cha Taifa fanya hima kuysajili upate namba ya kitambulisho ili usikatiwe mawasiliano ifikapo Desemba 31, 2019,” imehimiza taarifa ya TCRA.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC, SILABU waungana kufikisha elimu ya fedha majumbani

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeingia makubaliano ya ushirikiano...

AfyaHabari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Kisukari cha mimba ni nini?

Spread the loveKisukari cha mimba ni aina ya kisukari kinachotokea kwa baadhi...

Habari Mchanganyiko

Mafunzo kwa bodaboda 395 yamkuna Meya Dodoma

Spread the loveNAIBU Meya wa Jiji la Dodoma, Asma Karama amepongeza mafunzo...

Habari Mchanganyiko

Samia aagiza huduma za dharura maeneo yaliyoathiriwa na kimbunga Hidaya

Spread the love   RAIS wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Samia...

error: Content is protected !!