Saturday , 20 April 2024
Home Kitengo Maisha Afya Muuguzi anayedaiwa kumbaka mjamzito asimamishwa kazi
AfyaHabari Mchanganyiko

Muuguzi anayedaiwa kumbaka mjamzito asimamishwa kazi

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu
Spread the love

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amemsimamisha kazi Abednego Alfred, Muuguzi katika Kituo cha Afya cha Mamba, anayetuhumiwa kumbaka mama mjazito. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Waziri Ummy amechukua hatua hiyo leo tarehe 20 Desemba 2019, akiwa wilayani Mpanda, Mkoa wa Rukwa.

Aidha, Waziri Ummy ameliagiza Baraza la Wauguzi na Ukunga nchini, kusimamisha leseni ya Alfred, wakati uchunguzi wa tuhuma dhidi yake, ukiendelea kufanyika.

“Naliagiza baraza la wauguzi na ukunga kusimamisha leseni ya muuguzi huyu, wakati uchunguzi unafanyika,” ameagiza Waziri Ummy.

Wakati huo huo, Waziri Ummy amewaonya watumishi wa afya kutokiuka viapo vya maadili yao ya kazi na sheria.

“Na yeyote atakayefanya kazi kinyume na maadili, weledi na kiapo chake tutamchukulia hatua za kinidhamu. Ikewemo kuwafutia leseni zao na kuwapeleka katika vyombo vya dola”Amesisitiza Waziri Ummy.

Tukio linadaiwa kutokea tarehe 18 Desemba 2019, ambapo mAlfred anadaiwa kumbaka mama mjazito aliyekwenda katika Kituo cha Afya cha Mamba, kwa ajili ya kupata huduma ya kujifungua.

Inadaiwa kuwa, wakati mama mjazito huyo akiugulia maumivu ya uchungu, ndipo mtuhumiwa alipoitumia nafasi hiyo kumuingilia, hali iliyomfanya mama huyo kushtuka, ndipo alipomuona Alfred anamfanyia kitendo hicho cha ukatili.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

error: Content is protected !!