Monday , 6 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Wasiojulikana wadaiwa kumteka mtumishi wa LHRC
Habari Mchanganyiko

Wasiojulikana wadaiwa kumteka mtumishi wa LHRC

Wakili Tito Magoti, Mtumishi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC)
Spread the love

WAKILI Tito Magoti, mtumishi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), anadaiwa kukamatwa na watu wasiojulikana, asubuhi ya leo tarehe 20 Desemba 2019. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Taarifa za kukamatwa kwa wakili huyo, zilianza kutolewa na Mwanaharakati Bob Chacha Wangwe, kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Kwa mujibu wa Wangwe, Tito amekamatwa na watu watano waliovaa mavazi ya kiraia maeneo ya Mwenge jijini Dar es Salaam, ambapo walimuingiza kwa nguvu katika gari aina ya Harrier na kuondoka naye kusikojulikana.

MwanaHALISI ONLINE imemtafuta Anna Henga, Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, kwa ajili ya ufafanuzi wa tukio hilo, ambapo amekiri kupokea taarifa hizo.

Henga amesema wamefikisha taarifa hizo kwenye Kituo cha Polisi cha Mburahati jijini Dar es Salaam, ambapo wameelezwa kwamba, Tito hashikiliwi kituoni hapo.

Kiongozi huyo wa LHRC amesema Polisi wameahidi kufanya uchunguzi wa tukio hilo.

“Tumeenda Kituo cha Polisi cha Mabatini ambacho ndio kituo kikubwa, wamesema hawana taarifa za kukamatwa Tito, bali watachunguza tukio hilo. Wametuambia na sisi tuendelee kumtafuta,” amesema Henga.

Mtandao huu ulimtafuta Kamanda Musa Taibu, Kamanda wa Jeshi la Polisi Kinondoni, kwa ajili ya kufahamu  taarifa zaidi kuhusu kutekwa kwa mwanaharakati huyo, lakini jitihada hizo hazikufanikiwa.

Badala yake, alipokea mtu aliyejitambulisha kuwa ni msaidizi wake, na kueleza kwamba, Kamanda Taibu yuko msikitini, hivyo atafutwe baada ya swala.

Wakili Tito anayefahamika zaidi kama Mwanaharakati wa Haki za Binadamu, amekuwa akitumia ukurasa wake wa Twitter kuikosoa serikali.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mahakama yatoa uamuzi zuio dhidi ya Club House

Spread the loveMAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu jijini Dar es Salaam,...

Habari Mchanganyiko

GGML, OSHA yawanoa bodaboda 200 Arusha

Spread the loveZAIDI ya madereva bodaboda 200 wa jiji la Arusha wamepatiwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Serikali kuwakopesha wajasiriamali 18.5bn/- kupitia NMB

Spread the loveSerikali imetenga kiasi cha Sh 18.5 bilioni kwa ajili ya...

AfyaHabari Mchanganyiko

Huduma za kibingwa zazinduliwa katika hospitali za halmashauri 184

Spread the loveSERIKALI imezindua huduma za matibabu za kibingwa katika hospitali 184...

error: Content is protected !!