Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Ujumbe mzito wa Mbowe kwa Mnyika, Mwalimu na Kigaila
Habari za Siasa

Ujumbe mzito wa Mbowe kwa Mnyika, Mwalimu na Kigaila

Safu mpya ya Uongozi wa Chadema
Spread the love

FREEMAN Mbowe, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) amewapa ujumbe mzito, John Mnyika, Katibu Mkuu, Benson Kigaila, Naibu Katibu Mkuu Bara, na Salum Mwalimu, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Wakati akitangaza kuwateua Makatibu hao, leo tarehe 20 Desemba 2019 jijini Dar es Salaam, Mbowe amewaeleza kwamba, hajawateua kwa ajili ya kufanya starehe, bali kuzunguka nchi nzima kwa ajili ya kufanya kazi ya  kuimarisha Chadema.

Mbowe amewaeleza kuwa, hataki kuwaona makatibu hao wanajifungia kwenye ofisi za makao makuu ya Chadema, huku akisistiza kuwa, atawapelekesha ili wafanye kazi za chama hicho.

“Sijamteua ndugu Kigaila afikiri kuna sherehe na fiesta, nimemteua ndugu Kigaila, na nawaomba mumpokee, kwa sababu kati ya sasa na uchaguzi mkuu sitaki kumuona makao makuu. Zoezi la Chadema ni msingi, ambalo ndilo majivuno yetu ya leo, lazima liendelezwe kwa nguvu na wivu mkubwa,” ameeleza Mbowe.

Aidha, Mbowe ametaja sifa na vigezo alivyotumia kumteua Mnyika kuwa Katibu Mkuu, Kigaila kuwa Naibu Katibu Mkuu Bara, pamoja na kumrudisha Mwalimu kuwa Naibu Katibu Mkuu Zanzibar.

Mbowe amesema amewateua kwa kuwa wamekulia ndani ya Chadema, na wamekomazwa kisiasa wakiwa ndani ya chama hicho.

“Safari ya siasa ni safari ya mafunzo, nilioamua kuwateua safari hii, ni watu ambao tunawaamini pasipo shaka wamekulia ndani ya chama chetu, wamekomaa ndani ya chama chetu, “ amesema Mbowe.

Kiongozi huyo wa Chadema amesema amemrudisha Mwalimu, kutokana na kuridhishwa na utendaji kazi wake.

“Natambua kazi kubwa iliyofanywa na Naibu Katibu Mkuu Zanzibar anayemaliza muda wake Salum Mwalimu, amejitoa sana amefanya kazi sana visiwani na bara. Binafsi naheshimu sana mchango wake kwenye chama chetu, bado naamini tunahitaji kuendelea kumtumia,” amesema Mbowe.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia kutunukiwa udaktari wa heshima Uturuki

Spread the loveBaraza la Chuo Kikuu cha Ankara, ambacho ni cha pili...

error: Content is protected !!