Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Ni kazi kubwa kutenda haki – Ally Hapi
Habari za Siasa

Ni kazi kubwa kutenda haki – Ally Hapi

Spread the love

ALLY Hapi, Mkuu wa Mkoa wa Iringa amesema, kazi kubwa zaidi katika uongozi hasa wa kuteuliwa ni kutenda haki. Anaripoti Hamis Mguta, Iringa … (endelea).

Hapi ametoa kauli hiyo leo tarehe 2 Novemba 2019, katika Mkutano wa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi wakati wa kusikiliza kero za wananchi zinazogusa wizara hiyo.

“Waziri, watu hawa ukiwatendea haki kwa kazi unayofanya hii, Mungu anakubariki. Katika nafasi zetu hizi za uongozi, kazi kubwa na ngumu ya kufanya ni kutenda haki.

“Huu ndio mtihani mkubwa wa uongozi hasa sisi viongozi wa kuteuliwa, unakuwaje ni DC ambaye wananchi wako wanalia machozi na kudhulumiwa haki zao? na wewe ukasema mimi ni Mkuu wa Wilaya,” amesema.

“Najua kazi hizi zina changamoto na zina majungu, fitina, zina husda na jinsi pekee ya kujilinda na hayo ni kufanya haki kwa watu wanyonge,” amesema na kuongeza;

“Leo kuna mzee alikuja kunishukuru baada ya kumsaidia mgogoro wake wa kiwanja na akaniambia, amekuja kwa hilo tu na wala hajaja kuomba chochote, mimi nikupongeze unafanya kazi kubwa.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!