Thursday , 18 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Prof. Safari: Bila tume huru, ni vigumu kuingia Ikulu
Habari za SiasaTangulizi

Prof. Safari: Bila tume huru, ni vigumu kuingia Ikulu

Spread the love

PROF. Abdallah Safari, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), amedai kuwa vyama vya upinzani nchini, haviwezi kuingia Ikulu, bila kuwapo tume huru ya uchaguzi. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

 Akizungumza na MwanaHALISI ONLINE ofisini kwake, jijini Dar es Salaam, leo tarehe 2 Desemba 2019, Prof. Safari alisema, “upinzani unataka kwenda Ikulu, lakini bila kufuata njia ya kufika Ikulu.”

Amesema, “nimekatishwa tamaa na kinachofanywa na upinzani nchini. Nilipojiunga na upinzani nilitaka kusaidia kuing’oa madarakani Chama Cha Mapinduzi (CCM). Lakini naona dhamira hiyo kama haipo.” 

Prof. Safari amekuwa makamu mwenyekiti wa Chadema kwa miaka Saba, akichukua nafasi ya Said Alfi, aliyechukua nafasi hiyo kutoka kwa Chacha Zakayo Wangwe.

Akijibu swala la MwanaHALISI kuhusu sababu za kutogombea nafasi ya umakamu mwenyekiti wa Chaadema, Prof. Safari amesema, upinzani umemchosha. 

“Hiko kitu kimekuwa kinanikatisha tamaa sana; nimekuja Chadema vilevile sikuona kama kuna msukumo wa kupata tume huru ya uchaguzi, kwa hiyo tunataka kwenda Ikulu bila njia ya kwenda Ikulu,” ameeleza.

Amesema, “kutokana na hali hiyo, nimeona nipumzike siasa. Siwezi kwenda CCM kwa kwa sababu hawanipendi na mimi siwapendi.”

 Amesema, alimjulisha mwenyekiti wake, Freeman Mbowe, uamuzi wake wa kutogombea tena nafasi hiyo. Ametaja sababu ya kutogombea tena nafasi hiyo, kuwa ni pamoja na umri wake. 

Amesema, “nilimjulisha Mbowe kuwa sitagombea tena nafasi hii, mara baada ya matokeo ya Bunge la Afrika Mashariki, kwa sababu sikufurahishwa na mchakato ulivyofanyika.

“Unajua mimi nina miaka 68, nimekuwa kwenye upinzani kwa miaka miaka 20 sasa; na kwamba kabla ya kuingia huku, nilikuwa mkurugenzi Chuo cha Diplomasia, ambako niliachishwa kazi kwa sababu ya kumtetea Prof. Ibrahim Lipumba.”

Amesema, alitegema wapinzani wangekuwa na nguvu ya kuiangusha CCM, na hiyo ndio ilikuwa ajenda yake ya kuingia Chadema.

Prof. Safari ambaye pia ni wakili wa mahakama kuu na mmoja wa washauri wa mahakama ya rufaa amesema, aliwahi kumueleza Lipumba, mara baada ya uchaguzi wa mwaka 1995, “kwamba bila tume huru, hakuna uchaguzi huru.”

Anasema, hata Tume ya Jaji Francies Nyalali imeeleza kuwa uchaguzi wa vyama vingi, ni lazima utanguliwe na tume huru ya uchaguzi.

Alipoulizwa juu ya demokrasia ndani ya chama chake, Prof. Safari amesema, “hilo niliache kwa muda. Nitalizungumza baadaye. Lakini nafikiri tuna haja ya kuboresha demokrasia yetu ili tuwe na mamlaka ya kuisema CCM.”

Prof. Safari ameahidi kueleza umma muda siyo mrefu, hasa juu ya kilichompata aliyekuwa mwenyekiti wa Chadema, Kanda ya Pwani, Fredrick Sumaye.

Sumaye aliyekuwa mgombea pekee wa nafasi hiyo, alishindwa kutetea kiti chake, baada ya kupigiwa kura nyingi za hapana. 

Mwanasiasa huyu mahiri nchini anasema, wapigakura waliamua kumuadhibu kutokana na uamuzi wake wa kujitosa katika kiti cha uenyekiti wa taifa unaoshikiliwa na Mbowe.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

error: Content is protected !!