Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Msigwa amtumia ‘Yesu’ kujitetea kortini 
Habari za Siasa

Msigwa amtumia ‘Yesu’ kujitetea kortini 

Viongozi wa Chadema wakijadiliana na wakili wao mahakamani Kisutu katika muendelezo wa kesi yao
Spread the love

PETER Msigwa, Mbunge wa Iringa mjini, ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam kwamba amefunguliwa mashitaka ya uongo kama ilivyokuwa kwa Yesu Kristo. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Ametoa kauli leo tarehe 2 Desemba 2019, wakati akihojiwa na upande wa mashtaka (Jamhuri) ulioongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi akisaidiwa na Wakili wa Serikali Mkuu Joseph Pande, Wakili Mwandamizi Wankyo Simon na Wakili Jackiline Nyantori.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, Msigwa ambaye ni shahidi wa pili kwa upande wa utetezi, amedai mashitaka ya uchochezi katika kesi namba 112/2018 aliyofunguliwa yeye na wenzake wanane wa Chadema kwenye mahakama hiyo, yanalingana na yali aliyoshitakiwa Yesu.

Wakili Nchimbi alimuuliza, kwamba kwenye hadhara ya mahakama hiyo wapo waumini wa dini ya Kikristo anaowaongoza kwenye kanisa lake, kutokana na kile alichoeleza yeye ni mchungaji kwenye Kanisa la Viniyard, Msigwa amejibu “sina uhakika.” Mahojiano yalikuwa kama ifuatavyo;-

Wakili Nchimbi: Ni kweli kwenye historia Yesu Kristo aliwahi kufunguliwa mashtaka?

Msigwa: Ndio, alifunguliwa mashtaka ya uongo.

Wakili Nchimbi: Miongoni mwa mashtaka yake ni kujiita mfalme wa Wayahudi?

Msigwa: Yes, aliambiwa anafanya uchochezi.

Wakili Nchimbi:  Ni sahihi pia mashtaka aliyofunguliwa ni kujiita mwana wa Mungu?

Msigwa: Ni kweli.

Wakili Nchimbi: Mashtaka hayo bila shaka yalisikilizwa mbele ya Pilato, alipoulizwa kuhusu tuhuma za kujiita mfalme wa wayahudi alisemaje?

Msigwa: Wewe wasema.

Wakili Nchimbi:  Wakati wakili Kibatala anakuongoza ulisema umeshtakiwa kama Yesu?

Msigwa: Sijasema hivyo, nilisema wakati ule wa bibilia Yesu alifunguliwa mashtaka ya uongo kama nyinyi mlivyotufungulia mimi na wenzangu.

Msigwa akahojiwa na Wakili Wankyo:

Wakili Wankyo: Kwa mujibu wa  ushahidi wako, uliwataja watu mbalimbali wameuawa na wengine kujeruhiwa na ulimtaja Lissu ukasema amepigwa risasi,  wewe ulikuwepo wakati anapigwa?

Msigwa: Sikuwepo.

Wakili Wankyo: Ni sahihi kuwa hukuwahi kutoa taarifa kwenye kituo chochote cha polisi?

Msigwa:  Kwenye tukio la Lissu, polisi tulikuwa nao kabisa.

Wakili Wankyo: Narudia swali, uliwahi kutoa maelezo polisi au hukutoa?

Msigwa: Nilitoa  kuhusu tukio la Lissu.

Wakili Wankyo: Katika maelezo yako, uliwahi kuwataja watu waliofanya hilo tukio?

Msigwa: Sikuwaona.

Wakili Wankyo: Wewe unasema hukuwaona kuna mtu mwengine aliotoa maelezo kuhusu kuwaona?

Msigwa: Sijui.

Hata hivyo Msigwa aliiulizwa juu ya mauaji ya Akwelina akasema haya:-

Wakili Nyantori:  Ulizungumzia kifo cha mtu anayeitwa Akwelina kupitia taarifa ulizosikia amefariki wapi?

Msigwa: Kwa mujibu wa Mambosasa na Simon Sirro, Akwelina ameuawa Kinondoni.

Wakili Nyantori: Ni sahihi kwamba huyo Akwelina alikuwa kwenye mkusanyiko?

Msigwa: Sijasema hivyo, nilimsikia IGP Sirro anasema ni uzembe wa Jeshi la Polisi la wajitathimini.

Mbali na Msigwa kwenye shauri hilo, mshtakiwa mwengine ni Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema – Taifa; Dk. Vicent Mashinji, Katibu Mkuu wa Chadema; John Mnyika, Naibu Katibu Mkuu Chadema – Bara; Salum Mwalimu, Naibu Katibu Mkuu Chadema-Zanzibar.

Wengine ni pamoja John Heche, Mbunge wa Tarime Vijijini; Ester Matiko, Mbunge wa Tarime Mjini na Halima Mdee, Mbunge wa Kawe.

Washtakiwa wote  wanatuhumiwa kwa makosa 13, wanayodaiwa kuyafanya tarehe 16 Februali 2019, ikiwemo kufanya kufanya uchochezi, kusanyiko lisilo halali na maandamano yaliyosababisha kifo cha mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwelina Akwelin.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

CCM yakemea ufisadi, yaipa kibarua TAKUKURU

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimekemea vitendo vya ubadhirifu wa...

Habari za Siasa

Bajeti ya Ikulu 2024/25 kuongezeka, bunge laombwa kurudhia Sh. 1.1 trilioni

Spread the love  WIZARA ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa...

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

error: Content is protected !!