Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Waziri Jafo aanza kuandamwa 
Habari za Siasa

Waziri Jafo aanza kuandamwa 

Chiku Abwao ambaye ni Mwenyekiti wa Wanawake wa Chama cha ACT-Wazalendo – Taifa
Spread the love

SELEMANI Jafo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), sasa anashinikizwa kujiuzulu. Anaripoti Martini Kamote…(endelea).

Imeelezwa, ni kwa madai ya kushindwa kusimamia uchaguzi wa serikali za mitaa, na kusababisha vyama vya upinzani kuutelekeza kutokana na kuvurugwa na wasimamizi wake.

Akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 13 Novemba 2019, Chiku Abwao ambaye ni Mwenyekiti wa Wanawake wa Chama cha ACT-Wazalendo – Taifa amedai, Waziri Jafo anahusika katika kuvuruga uchaguzi.

“Inampasa ajiuzulu, ameshindwa kusimamia uchaguzi, ameamua kupuuza malalamiko ya vyama vyetu na kukibeba chama chake –CCM- kwa kuumiza vyama vyetu.

“Amekuwa akitoa kauli zenye kupingana, huo ni ushahidi tosha kwamba ameshindwa kazi, ili uchaguzi ufanyike kunahitajika usawa ambao chini ya uongozi wake, umeshindwa kupatikana, lakini cha ajabu amekubali kutumika,” amesema.

Amesema, kama uchaguzi huo utafanyika, Wanawake wa ACT-Wazalendo hawatawatambua na wala kutoa ushirikiano kwa viongozi watakaochaguliwa.

“Huu ni uchaguzi wa chama kimoja katika serikali inayojitangaza kuwa na mfumo wa vyama vingi, kati serikali haiwezi kujinasibu kwa kusimamia uchafu huu na kuubariki,” Abwao amemweleza mwandishi wa habari hii.

Amesema, uzoefu unaonyesha kuwa migogoro mingi, hasa ya kutumia nguvu huaathiri zaidi wanawake na watoto kuliko makundi mengine ya jamii.

“Tunawaomba  viongozi wetu wa chama kukutana na vyama vyote makini vya siasa, ili kuwa na msimamo wa pamoja katika hili la kufutwa uchaguzi huu,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!