Sunday , 5 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Wazee Morogoro waiangukia MORUWASA
Habari Mchanganyiko

Wazee Morogoro waiangukia MORUWASA

Bomba la maji
Spread the love

WAZEE mkoani Morogoro wameiomba Mamlaka ya maji safi na maji taka mkoa
(MORUWASA) kuhakikisha huduma ya maji inafika kila eneo ili kuwasaidia
wazee kuondokana na adha ya kukosa maji. Anaripoti Christina Haule, Morogoro … (endelea).

Mama Beatrice Mogera, mwakilishi kamati ya
wazee Manispaa ya Morogoro, kutoka Umoja wa wazee mkoani Morogoro (MOREPEO), amesema huduma ya maji katika baadhi ya maeneo mkoani Morogoro imekuwa
kitendawili ambacho kinapaswa kupatiwa ufumbuzi wa haraka.

“Sisi sasa ni wazee, tunaanza na hekaheka za kusaka yalipo maji, hamuoni kama tunasumbuka bure, MORUWASA ituonee huruma, iharakishe upatikanaji wa maji katika maeneo yetu kwa haraka,” alisema Mama Mogera.

Hata hivyo mama Mogera aliiomba Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro
kuona haja ya  kuanza kutekeleza ahadi ya 2 ya mikopo ya wazee iliyowekwa na Halmashauri ambayo imekuwa haitekelezeki toka
ilipopitishwa kwenye ilani ya Chama Cha Mapinduzi 2015/20.

Hivyo alisema, wazee na vijana wanayonafasi ya kushirikiana kutafuta ufumbuzi wa changamoto zinazowakumba wazee kiuchumi, kijamii na kiafya kufuatia wao nao kuelekea kwenye uzee hapo baadae.

Naye Mganga mkuu wa manispaa ya Morogoro Dk. Ikaji Rashidi aliwataka
wazee kutambua kuwa Manispaa inawajali katika suala zima la Afya na kwamba tayari wazee 4002 kati ya wazee 15,631 waliopo Manispaa wameshapatiwa vitambulisho vya matibabu bure ambavyo havina mwisho
kama ilivyo kwenye kadi za huduma ya Afya CHF.

Dk. Rashidi alisema, wameendelea kuboresha huduma za kwa wazee na kuhakikisha huduma za dawa zinapatikana kwa asilimia 92-98 na kwamba huduma ya upimaji wa magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo kisukari na
presha inapatikana bure siku ya Alhamisi kwenye kituo cha afya Sabasaba.

Akizungumza kwenye maadhimisho hayo mgeni rasmi, Katibu tawala msaidizi wa wilaya ya Morogoro, Yahya Naniya kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Morogoro Regina Chonjo alitoa wito kwa viongozi wa Halmashauri kuwaalika wazee wawili kutoka ngazi ya kata kuhudhuria katika vikao vya maendeleo ya kata na wazee wawili kuhudhuria katika
baraza la madiwani kama ilivyoelekezwa na Serikali.

Naniya alisema, maagizo hayo ya wazee kupata uwakilishi kwenye maeneo
hayo yalitolewa muda mrefu lakini yalikuwa hayatekelezwi na kuwafanya wazee kuendelea kulalamika kukosa uwakilishi kwenye maeneo yote jambo ambalo halikuwa na ukweli.

Hata hivyo aliipongeza Halmashauri ya Manispaa kwa kutenga huduma za
wazee na kuvitaka vituo vingine vya Afya mkoani hapa kuiga mfano wa Manispaa ya Morogoro kwa usogeza huduma hizo muhimu walipo wazee.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga Hidaya chatikisa Mafia

Spread the loveWAKATI hali ya upepo mkali ikiendelea kushuhudiwa katika baadhi ya...

Habari MchanganyikoTangulizi

Usafiri baharini wasitishwa kukwepa athari za kimbunga Hidaya

Spread the loveUSAFIRI wa baharini umesimamishwa kwa muda ili kukwepa athari za...

Habari Mchanganyiko

RPC Dodoma akabidhiwa bunduki mbili za wahalifu

Spread the love  Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa ya Kulevya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yazindua huduma maalum kwa wastaafu

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua huduma maalum kwa...

error: Content is protected !!