Friday , 29 September 2023
Home Habari Mchanganyiko Tumezima tukio la ujambazi -Kamanda Mambosasa
Habari Mchanganyiko

Tumezima tukio la ujambazi -Kamanda Mambosasa

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa
Spread the love

JESI la Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam limeeleza kufanikiwa kuzima tukio la ujambazi, Mbezi Msakuzi, njia panda ya Mpiji Magoe. Anaripoti Kamote…(endelea).

Limeeleza, mafanikio hayo yametokana na taarifa kutoka  kwa raia wema kwamba, kulikuwepo mpango wa kuvamia Saccoss ya Msakuzi tarehe 26 Septemba 2019.

Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 10 Oktoba 2019 na Lazaro  Mambosasa, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam wakati akizungumza na wanahabari.

“Jeshi la Polisi, Kanda Maalumu Dar es Salaam kupitia kikosi kazi kilichokuwa  kimeweka mtego, na ilipofika majira ya saa sita mchana zilifika pikipiki mbili aina ya boxer ambazo hazikusomeka namba zikiwa na majambazi wane.

“Mmoja kati yao akiwa na bastola, ndipo  walipoona polisi na kuanza kukimbia huku wakirushiana risasi, lakini askali mahiri walipofanikiwa kuwajeruhi wawili,” amesema.

Amesema, majeruhi hao walipopekulia, walikutwa na bastola moja, risasi tatu ndani ya magazine na maganda mawili ya risasi ambapo walipelekwa hospitali na baadaye kufariki.

“Jeshi la Polisi, Kanda Maalumu, kupitia kikosi kazi chake kimefanikiwa pia kumuua jambazi hatari aliyekuwa anatafutwa kwa muda mrefu kwa kufanya matukio mbalimbali ya mauaji na ujambazi.

“Tarehe 30 Septemba 2019 saa saba mchana, Jeshi la Polisi lilipta taarifa kutoka kwa msiri wake kuwa, Ilala Boma kuna jambazi sugu anayefahamika ka jina la Emmanuel Peter maarufu kwa jina la Mark Silengo na wenzake wanne, wanapanga mipango ya kwenda kufanya uhalifu,’ amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Maabara ya bilioni 5 upimaji madini yazinduliwa Geita, inapima kwa mionzi

Spread the loveZaidi ya Sh bilioni tano zimewekezwa katika kampuni ya MSALABS...

ElimuHabari Mchanganyiko

Wanafunzi Nyamkumbu wanolewa na GGML kuhusu taaluma ya madini

Spread the loveZAIDI ya Wanafunzi 50 kutoka Shule ya Sekondari ya Wasichana...

Habari Mchanganyiko

Somo la dini: Waislamu waishukia Serikali, wizara yatoa kauli

Spread the loveJUMUIYA na Taasisi za Kiislamu Tanzania, imetupia lawama Serikali ikidai...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga: Usambazaji umeme vijijini mwisho Desemba 2023

Spread the love  NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema ifikapo mwezi...

error: Content is protected !!