Sunday , 5 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Dk. Bashiru: Kweli vyuma vimekaza
Habari za Siasa

Dk. Bashiru: Kweli vyuma vimekaza

Spread the love

DAKTARI Bashiru Ally, Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), amesema “ni kweli vyuma vimekazi” akaongeza “kwa wale wapiga dili.” Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Kiongozi huyo wa chama tawala, yumo jijini Dar es Salaama akiendelea na ziara yake ya kichama katika Jimbo la Ubunge linaloongozwa na Saed Kubenea (Chadema) ikiwa ni siku yake ya pili.

Akizungumza leo tarehe 28 Agosti 2019 katika Shule ya Msingi Ubungo Kisiwani Dk. Bashiru amesema, ni wakati wa kufanya kazi na sio kukaa ‘vijiweni’ kwamba wale wasiokuwa na kazi maalumu wataendelea kulalamika.

“Vijana waachane na tabia ya uvivu kwani uvivu ni adui wa maendeleo… muda wa kupata dezo umepita,” amesema Dk. Bashiru na kuongeza; “vijana muache kukatishana tamaa.”

Amesema, ikiwa vyuma vimekazwa kwa sababu ya kujenga shule, kuokoa vifo vya kina mama, kulina uhuru na amani bado vyuma hivyo viendelee kukaza mpaka Watanzania tushike adabu.

Dk. Bashiru anaendelea na ziara yake kwenye jimbo hilo, ambapo baadaye ataanza ziara katika jimbo la Kibamba linaloongozwa na John Mnyika (Chadema).

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mbatia ambwaga Selasini, mahakama yaamuru alipwe fidia

Spread the loveMAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imemuamuru...

Habari za SiasaTangulizi

Mkulo afariki dunia, kuzikwa kesho Kilosa

Spread the loveALIYEKUWA Waziri wa Fedha na Mbunge wa Kilosa (CCM), Mustafa...

Habari za SiasaTangulizi

Sabaya afutiwa kesi, ruksa kugombea uongozi

Spread the loveMwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP leo Ijumaa amefuta rufaa...

Habari za Siasa

Serikali yasaka bilioni 3 kujenga daraja Mto Mpiji

Spread the loveSerikali imesema inaendelea na juhudi za kutafuta fedha kiasi cha...

error: Content is protected !!