Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Polisi wamng’ang’ania Mdee
Habari za Siasa

Polisi wamng’ang’ania Mdee

Halima Mdee, Mbunge wa Kawe
Spread the love

JESHI la Polisi mkoani Kagera, bado linamshikilia Halima Mdee, Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bawacha), tangu jana tarehe 14 Julai 2019. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Kwa mujibu wa Tumaini Makene ambaye ni msemaji wa chama hicho, Mdee bado yupo mikononi mwa polisi kwa tuhuma za kufanya uchochezi.

Mdee ambaye pia ni Mbunge wa Kawe, jijini Dar es Salaam, Grace Tendega ambaye ni Katibu wa Bawacha, Conchesta Rwamlaza; Mwenyekiti wa Bawacha Mkoa wa Kagera na Anatropia Theonest; Mbunge Viti Maalum waliitwa katika Kituo cha Polisi cha Bukoba kuhojiwa.

Baada ya mahojiano hayo, ni Mdee pekee yake alinyimwa dhamana huku viongozi wengine wakiachwa.

“Polisi wanaendelea kumshikiria Mdee wakidai kuwa, wanasubiri maelekezo kutoka kwa Kamanda wa Mkoa wa Kagera aliyekuwa kwenye ziara ya Rais John Magufuli kwamba wamuachie kwa dhamana au wamfikishe mahakamani,” taarifa hiyo ya Chadema imeeleza.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

error: Content is protected !!