RAIS John Magufuli, Amiri Jeshi Mkuu wa Nchi, ameonya wanasiasa wanaodhalilisha vyombo vya ulinzi na usalama nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa nyumba za polisi mkoani Geita leo tarehe 15 Julai 2019, Rais Magufuli amewataka wanasiasa kujiepusha na tabia ya kutoa maneno yanayodhalilisha vyombo hivyo.
Ameeleza kuwa, wanasiasa hao hutoa maneno hayo kwa vyombo vya ulinzi na usalama kwa ajili ya kutafuta sifa na umaarufu kwa wananchi.
“Nawasihi wanasiasa wenzetu tujiepushe na tabia ya kutoa maneno yanayodhalilisha vyombo vya ulinzi na usalama kwa lengo la kujitafutia sifa na umaarufu kwa wananchi,” amesema Rais Magufuli.
Wakati huo huo, Rais Magufuli ameagiza Jeshi la Polisi kujipanga kwa ajili ya kusimamia uchaguzi wa serikali za kitaa unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu.
“Kusisitiza umuhimu wa jeshi kuendelea kujipanga katika kipindi ambacho nchi yetu inajiandaa na uchaguzi wa serikali za mitaa,” ameagiza Rais Magufuli.
Kuhusu uzinduzi wa nyumba hizo, Rais Magufuli ameipongeza Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi pamoja na Jeshi la Polisi kwa kufanikisha utekelezaji wa ujenzi wa nyumba hizo.
Aidha, ameliagiza Jeshi la Polisi kuhakikisha kwamba ujenzi wa nyumba unamalizika kwa wakati.
Leave a comment