Friday , 29 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Hatuogopi uchaguzi Singida, tunakataa uharamu – Chadema  
Habari za SiasaTangulizi

Hatuogopi uchaguzi Singida, tunakataa uharamu – Chadema  

Tundu Lissu, mgombea wa Urais wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020 kwa tiketi ya Chadema
Spread the love

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema, “kushiriki uchaguzi mdogo katika jimbo la Singida Mashariki, ni sawa na kutenda uovu.” Anaripoti Hamis Mguta…(endelea).

Uchaguzi mdogo katika jimbo la Singida Mashariki, lililokuwa likiongozwa na Tundu Lissu, unatarajiwa kufanyika tarehe 31 Julai 2019.

Tume ya Taifa ya uchaguzi (NEC), imetangaza kufanyika uchaguzi huo, kufuatia Spika wa Bunge, Job Ndugai, kutangaza kumvua Lissu ubunge wake, tarehe 28 Juni mwaka huu, wakati wa kuhitimisha mkutano wa Bunge la Bajeti.

Akizungumza na MwanaHALISI ONLINE, leo Jumatatu, tarehe 15 Julai, afisa wa habari wa chama hicho, Tumaini Makene amesema, kwa chama chake, kushiriki uchaguzi huo, ni sawa na kuunga mkono kitendo cha Spika Ndugai kumvua ubunge Lissu.

“Tunakwenda mahakamani, kupigania haki ya wananchi wa Singida Mashariki na wananchi wengine kwa ujumla. Tunakwenda mahakamani kutetea demokrasia na kupinga maamuzi yaliyofanywa na Ndugai na watu wake,” ameeleza Makene.

Alipoulizwa ni lini hasa kesi hiyo itafuguliwa, afisa habari huyo wa Chadema amesema, “mchakato upo kwenye hatua nzuri. Tutawasilisha kesi hii mapema iwezekanavyo ili kuwaondoa wasiwasi wanachama wetu.”

Makene anasema, kumekuwa na muendelezo wa hila katika ubunge wa Lissu hadi kupelekea hata NEC, kuweka muda mchache wa maandalizi ya uchaguzi huo.

“Unaweza kuona hata kwenye ratiba ya NEC wameweka siku 12 za kampeni,” anaeleza na kuhoji, “inawezekanaje kampeni ya kumtafuta mbunge zikafanyika ndani ya siku 12, wakati hata mwenyekiti wa serikali ya mtaa na kitongoji, ni siku 21?”

Wiki iliyopita, NEC ilitangaza kuwa uchaguzi mdogo katika jimbo la Singida Mashariki, utafanyika tarehe 31 Julai 2019, huku ikieleza kuwa ratiba yake inatokana na barua ya Spika Ndugai inayoeleza kuwa aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Tundu Antipas Lissu, amepoteza sifa ya kuwa mbunge.

Lissu ambaye ni mmoja wa wanasheria mashuhuri nchini, alitangazwa kuvuliwa ubunge wakati akiwa nje ya nchi kwenye matibabu.

Mwanasiasa huyo, amekuwa nchini Ubelgiji tangu mwanzoni mwa mwaka jana, kufuatia kushambuliwa kwa risasi akiwa nyumbani kwake, eneo la Area D mjini Dodoma, tarehe 7 Septemba 2017.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Serikali yawaangukia viongozi wa dini

Spread the loveSERIKALI imewaomba viongozi wa dini, waendelee kuelimisha wananchi kudumisha amani...

Habari MchanganyikoTangulizi

Afya ya akili yatajwa chanzo kuvunjika ndoa

Spread the loveCHANGAMOTO ya afya ya akili, imetajwa kuwa chanzo cha migogoro...

Habari za Siasa

Azzim Dewji aitaka Serikali iwanyooshe mafisadi

Spread the loveMFANYABIASHARA maarufu nchini, Azzim Dewji, ameitaka Serikali iwachukulie hatua wezi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga: Usambazaji umeme vijijini mwisho Desemba 2023

Spread the love  NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema ifikapo mwezi...

error: Content is protected !!