
Halima Mdee, Mbunge wa Kawe
JESHI la Polisi mkoani Kagera, bado linamshikilia Halima Mdee, Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bawacha), tangu jana tarehe 14 Julai 2019. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).
Kwa mujibu wa Tumaini Makene ambaye ni msemaji wa chama hicho, Mdee bado yupo mikononi mwa polisi kwa tuhuma za kufanya uchochezi.
Mdee ambaye pia ni Mbunge wa Kawe, jijini Dar es Salaam, Grace Tendega ambaye ni Katibu wa Bawacha, Conchesta Rwamlaza; Mwenyekiti wa Bawacha Mkoa wa Kagera na Anatropia Theonest; Mbunge Viti Maalum waliitwa katika Kituo cha Polisi cha Bukoba kuhojiwa.
Baada ya mahojiano hayo, ni Mdee pekee yake alinyimwa dhamana huku viongozi wengine wakiachwa.
“Polisi wanaendelea kumshikiria Mdee wakidai kuwa, wanasubiri maelekezo kutoka kwa Kamanda wa Mkoa wa Kagera aliyekuwa kwenye ziara ya Rais John Magufuli kwamba wamuachie kwa dhamana au wamfikishe mahakamani,” taarifa hiyo ya Chadema imeeleza.
More Stories
Tutaenzi maono ya Rais Magufuli – Waziri Majaliwa
Wavuvi kicheko, TAFICO kufufuliwa
Tozo za bandari kupitiwa upya