Tuesday , 30 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Maalim Seif, Zitto waivaa Ukonga
Habari za Siasa

Maalim Seif, Zitto waivaa Ukonga

Spread the love

ZITTO Kabwe, Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo na Maalim Seif Sharif Hamad, mwanachama namba moja wa chama hicho, walilivaa Jimbo la Ukonga na kuchota wanachama wapya. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Walianza ziara kwenye jimbo hilo jioni ya tarehe 30 Mei 2019, ambapo Zitto na Maalim Seif walizungumza na wanachahama huku wakifungua matawi sambamba na kupokea wanachama wapya.

Kwenye ziara hiyo Zitto alisema, nchi inahitaji kupumua na njia pekee ni kuhakikisha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinakaa pembeni.

Alitoa kauli hiyo baada ya kuulizwa na wanahabari juu ya mikakati ya ACT-Wazalendo kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa baadaye mwaka huu na Uchaguzi Mkuu mwakani.

Zitto na Maalim Seif walikwenda kuzindua ofisi mpya za chama hicho katika Jimbo la Ukonga, Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam ikiwa ni hatua za awali kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa.

“Chama chetu kipo kwa ajili ya kuhakikisha tunajenga ushirikiano na vyama vengine vya upinzani kwa lengo la kuleta mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi kwa wananchi. Hali ya maisha ya wananchi haiwezi kuwa bora zaidi bila kuwa pamoja kwa kushirikiana.

“Ili kuhakikisha yanatoke mabadiliko nchini na kuwa na maendeleo, CCM iondolewe. Ndio maana tunafanya kazi kwa pamoja kama nilivyowaeleza, tulikuwa na kikao cha vyama vinane vya  upinzani,” alisema Zitto.

Amesema kuwa, vyama nane vya upinzani vipo kwenye mjadala juu ya masuala mahususi yanayoweza kuleta mabadiliko kwenye nchi.

Pia vyama hivyo vinajadili uamuzi wa Mahakama Kuu kuhusu hukumu ya kesi ya Bob Chacha Wangwe, iliyozuia wakurugenzi wa halmashauri na manispaa kusimamia chaguzi.

“Na kama mnavyofahamu, ni miaka mine sasa ya serikali ya CCM chini ya Rais John Magufuli, hakuna watu ambao hawajaguswa na uamuzi mbovu, mmesikia wakulima wamelalamika, wakulima wa kada zote.

“Alianza na wakulima wa mbaazi wakapata hasara, wakulima wa korosho kama munavyosikia mpaka sasa bado jambo hili halijapata ufumbuzi, sasa hivi kuna kampuni kubwa ya tumbaku ya usindikaji wa tumbaku imepunguza wafanyakazi elfu tatu na imefunga ofisi zake Tanzania, wemesema wanaondoka kwasababu ya mazingira mabovu ya biashara hapa Tanzania” amesema Zitto.

Maalim Seif amewaeleza wakazi wa Chanika kuwa, ACT-Wazalendo haiwezi kufanikiwa kama hakutakuwa na umoja kati ya chama hicho na wananchi.

“Hakuna ambalo unaweza kulifanya pekee yako, mkishikamana mtafanya makubwa …lakini pia nidhamu, ni lazima chama chetu kiwe na nidhamu ya hali ya juu kabisa” amesema Maalim Seif.

Amesema kuwa, nidhamu, umoja na mshikamano kwa pamoja vitaiondoa CCM madaakani kwenye uchaguzi mkuu wa 2020. Amewataka wanachama wapya na wanaotaka kuwania uongozi kujizatiti kwa kuwa, upinzani una changamoto nyingi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

Habari za SiasaTangulizi

Samia ataja miradi ambayo Tanzania inashirikiana na IDA

Spread the loveRais wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan leo Jumatatu amehutubia...

error: Content is protected !!