Tuesday , 7 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Wanaume mnaonyanyaswa jitokezeni – Serikali
Habari Mchanganyiko

Wanaume mnaonyanyaswa jitokezeni – Serikali

Dk. Faustin Ndungulile
Spread the love

SERIKALI imewataka wanaume wanaonyanyaswa kijinsia na wake zao, kutoa taarifa kwenye madawati ya kijinsia. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 3 Mei 2019 na Faustine Ndugulile, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakati akijibu swali la nyongeza la Rita Kabati, Mbunge wa Viti Maalum (CCM).

Katika swali lake Rita Kabati ametaka kujua, serikali itatunga lini sheria ya kuwatetea wanaume wanaonyanyaswa kijinsia na wake zao?

Ndugulile amesema, yapo madawati yanayoshughulikia maswala ya unyanyasaji katika vituo vya polisi na maeneo mbalimbali.

Na kwamba, tatizo kubwa ni wanaume kutojitokeza kulalamikia vitendo hivyo badala yake hukaa kimya.

Akijibu swali la msingi la Mbunge wa Vitimaalum, Amina Makilagi (CCM), Ndungulile amesema, serikali inatambua ukatili wa kijinsia ni pamoja na vitendo vya kuwanyanyasa, kuwadhalilisha na kuwadhulumu wanawake na watoto.

Amsema, ukatili wa kingono na kisaikolojia ni sehemu ya ukatili wa kijinsia hivyo ni muhimu kutolewa taarifa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mahakama yatoa uamuzi zuio dhidi ya Club House

Spread the loveMAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu jijini Dar es Salaam,...

Habari Mchanganyiko

GGML, OSHA yawanoa bodaboda 200 Arusha

Spread the loveZAIDI ya madereva bodaboda 200 wa jiji la Arusha wamepatiwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Serikali kuwakopesha wajasiriamali 18.5bn/- kupitia NMB

Spread the loveSerikali imetenga kiasi cha Sh 18.5 bilioni kwa ajili ya...

AfyaHabari Mchanganyiko

Huduma za kibingwa zazinduliwa katika hospitali za halmashauri 184

Spread the loveSERIKALI imezindua huduma za matibabu za kibingwa katika hospitali 184...

error: Content is protected !!