Sunday , 28 April 2024
Home Kitengo Maisha Elimu Bodi ya Mikopo kukopesha wanachuo 128,285
ElimuHabari za Siasa

Bodi ya Mikopo kukopesha wanachuo 128,285

Bodi ya Mikopo Elimu ya Juu
Spread the love

BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), inatarajiwa kutoa mikopo kwa wanafunzi 128,285 sawa na ongezeko la asilimia 4.5 ikilinganishwa na mwaka wa fedha uliopita (2018/19). Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Kati yao, wanafunzi 45,485 watakuwa wa mwaka wa kwanza ikiwa ni ongezeko la silimia 10.3 ikilinganishwa na wanafunzi 41,234 wa mwaka 2018/19.

Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 29 Aprili 2019 bungeni na Prof. Joyce Ndalichako, Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia wakati akiwasilisha bungeni Makadilio ya Mapato na Matumizi ya Fedha kwa Mwaka 2019/2020.

Prof Ndalichako amesema kuwa, bodi hiyo itafuatilia fedha inayolipwa ili kuhakikisha fedha za mikopo zinawafikia kwa wakati wanafunzi stahiki.

Amesema, bodi hiyo imepanga kutekeleza mambo kadhaa ambayo ni kutoa mikopo yenye thamani ya Sh, 450 Bil ambapo ni ongezeko la asilimia 5.0 ikilinganishwa na mwaka 2018/19.

“Kukusanya Sh. 221.5 Bil kutoka kwa wanufaika ambao mikopo yaio imeiva, hili ni ongezeko la asilimia 40.5 ukilinganuisha na lengo la mwaka 2018/19 ambalo ni Sh. 157.7 Bil,” amesema.

Prof. Ndalichako amesema, HESLB itaanzisha na kuimarisha ofisi mbili za kanda katika Mikoa ya  Mbeya na Mtwara ili kufikisha jumla ya ofisi sita za kanda.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Sauti ya Watanzania waeleza sababu za kuiunga mkono Chadema

Spread the love  KIKUNDI kinachojipambanua katika kupigania rasilimali na uhuru wa nchi,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

error: Content is protected !!