HATUA ya wanaume wengi kudaiwa kutumia dawa za kuongeza nguvu za kiume, imegeuka mjadala bungeni huku wabunge wakiangua kicheko. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).
Katika kipindi cha maswali na majini leo tarehe 29 Aprili 2019, swali lililoulizwa na Godluck Mlinga, Mbunge wa Ulanga (CCM) kuhusu matumizi ya dawa za kuongeza nguvu za kiume, limeawaacha hoi wabunge.
Mlinga amehoji, ni sababu gani zinapelekea watu wengi kutumia dawa za kuongeza nguvu za Kiume?
Akiuliza swali la nyongeza bungeni, mbunge huyo amesema kuwa, kwa sasa kuna wimbi kubwa la dawa za kuongeza mguvu za kiume tofauti na ilivyokuwa kipindi cha nyuma.
“Kwa sasa kuna wimbi kubwa la dawa za kuongeza nguvu za kiume tofauti na ilivyokuwa kipindi cha nyuma, je ni kwani kumekuwepo kwa wingi wa dawa hizo? Ni sababu gani ambazo zinapelekea watu wengi kukosa nguvu za kiume?” amehoji Mlimnga.
Mbunge wa Viti Maalum, Suzan Lyimo (Chadema) akiuliza swali la nyongeza bungeni, amehoji serikali na kutaka ieleze ni madhara gani ambayo yanaweza kujitokeza kwa baadhi ya watu ambao wanatumia dawa za kuongeza ukubwa wa maumbile ya kiume (uume).
Awali katika swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalum, Rukia Kassim Ahamed (CUF) alitaka kujua kama serikali ipo tayari kufungia saloon zote pamoja na kuwachukulia hatua kali wale wote wanaotoa huduma hiyo.
Akijibu maswali hayo Wazili wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Hussein Mwinyi kwa Niaba ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto amesema, yapo madhara mengi ambayo yanatokana na matumizi ya dawa ambazo hazijadhibitiwa.
Kuhusu wanaume wengi kukosa nguvu za Kiume alisema kuwa zipo sababu mbalibali magonjwa kama vile kisukari pamoja na msongo wa mawazo.
Dk. Mwinyi amesema kuwa, pamoja na kuwepo kwa tatizo la kukosekana nguvu za kiume, ni vvyema wale wanaohitaji kutumia dawa hizo watumie ambazo zimethibitishwa.
Kuhusu wanaume kutumia dawa za kuongeza maumbile ya kiume Dk. Mwinyi amesema kuwa, mpaka sasa hana taarifa yoyote ya dawa ambayo inaweza kuongeza ukubwa wa maumbile hayo.
Amesema kuwa, watu wasitumie dawa yoyote na inatakiwa mtu yeyote anayetoa taarifa, atoe taarifa ambayo ni ya uhakika.
Kuhusu kufunga saloon za kike Dk. Mwinyi amesema, serikali haioni sababu ya kufungia wala kuwachukulia hatua wanaotoa huduma hiyo.
Na kwamba, bali wizara kupitia TFDA itaendelea kutoa elimu kwa watumiaji pamoja na kuhamasisha watendaji wa afya umuhimu wa kutoa taarifa za ubora na madhara yatokanayo na matumizi ya bidhaa za chakula, dawa, vipodozi.
Leave a comment