Sunday , 5 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Prof. Lipumba aeleza ‘jeuri’ ya kufanya mkutano mkuu
Habari za Siasa

Prof. Lipumba aeleza ‘jeuri’ ya kufanya mkutano mkuu

Prof. Ibrahim Lipumba
Spread the love

PROFESA Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa, ameeleza sababu za kufanyika kwa mkutano mkuu wa saba wa chama hicho, licha ya kuzuiliwa na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam. Anaripoti Hamisi Mguta … (endelea).

Akizungumza kwenye mkutano huo wa siku tatu unaofanyika katika ukumbi wa Lekam ulioko Buguruni jijini Dar es Salaam, Prof. Lipumba amesema kambi ya Maalim Seif Sharrif Hamad imeshindwa kuuzuia mkutano huo, kwa kuwa ilimshtaki yeye badala ya Baraza Kuu la Uongozi la CUF Taifa, linaloitisha mkutano huo.

Prof. Lipumba amedai kuwa, kambi ya Maalim Seif ambaye ni Katibu Mkuu wa CUF ilifanya makosa kumshitaki yeye pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa CUF Bara, Magdalena Sakaya, kwa kuwa, katiba ya chama hicho haikumtaja yeye na au mtu yeyote kwamba ana mamlaka ya kuitisha mkutano huo, isipokuwa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa.

“Leo mkutano huu ulitaka uzuiliwe lakini nashukuru kwa kiburi chake badala kufungua kesi dhidi ya baraza kuu akamshtaki Sakaya na Lipumba. Kwenye katiba ya CUF haieleza mkutano mkuu unaitishwa na Lipumba, mimi sijaitisha mkutano mkuu huu na wala msajili hana barua yangu ya kuitisha mkutano huu,” amesema Prof. Lipumba.

Prof. Lipumba amesema ilikuwa ngumu kufanikisha mkutano huo akieleza kwamba ulizungukwa na mizengwe na vizingiti.

“Wajumbe tuko hapa tunasali katika hali ilivyokuwa ngumu kufanikisha mkutano huu, haikuwa kazi ndogo kamati ya utendaji ilifanya kazi kubwa. Pamoja na mapungufu yote lakini tumefanikisha na hasa ukizingatia mizengwe na vizingiti vilivyowekwa,” amesema Prof. Lipumba.

Mwishoni mwaka mwaka jana, Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam mbele ya Jaji, Dk. Benhajj Masoud ilitoa amri ya kuhifadhi hali iliyopo katika chama cha CUF ikiwemo kuzuia kufanyika kwa mkutano mkuu ulioitishwa na Prof. Lipumba hadi pale shauri la msingi Na. 23/2016 litakapotolewa uamuzi.

Amri hiyo ilitolewa na mahakama baada ya Kambi ya Maalim Seif kupitia Naibu Katibu Mkuu wa CUF Bara, Joran Bashange na Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar, Nassoro Mazrui kufungua shauri dogo Na. 40/2018, kuiomba mahakama kuzuia kufanyika kwa mkutano huo hadi shauri la msingi linalohoji uhalali wa uenyekiti wa Prof. Lipumba litakapotolewa uamuzi.

Tazama video kamili hapo chini 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mbatia ambwaga Selasini, mahakama yaamuru alipwe fidia

Spread the loveMAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imemuamuru...

Habari za SiasaTangulizi

Mkulo afariki dunia, kuzikwa kesho Kilosa

Spread the loveALIYEKUWA Waziri wa Fedha na Mbunge wa Kilosa (CCM), Mustafa...

Habari za SiasaTangulizi

Sabaya afutiwa kesi, ruksa kugombea uongozi

Spread the loveMwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP leo Ijumaa amefuta rufaa...

Habari za Siasa

Serikali yasaka bilioni 3 kujenga daraja Mto Mpiji

Spread the loveSerikali imesema inaendelea na juhudi za kutafuta fedha kiasi cha...

error: Content is protected !!