April 14, 2021

Uhuru hauna Mipaka

‘Ulaji holela dawa za kupunguza maumivu ni hatari’

Dk. Faustin Ndungulile

Spread the love

ULAJI holela wa dawa za kupunguza maumivu ni moja ya sababishi ya ugonjwa wa Figo, imeelezwa. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 14 Machi 2019 na Dk. Faustine Ndungulile, Naibu Waziri wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto alipozungumza na waandishi wa habari katika Kilele cha Siku ya Figo Duniani.

Amesema, kumekuwa na ongezeko kubwa la wagonjwa wa figo hapa nchini kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ulaji wa dawa za maumivu kiholela.

“Kuna visababishi vingi lakini katika hizi dawa ambazo watu ujinwea bila ushauri wa daktari ni tatizo kubwa,” amesema.

Amesema, mpaka sasa tayari wagonjwa 42 wameshapandikizwa figo katika hospitali ya Benjamini Mkapa na Muhimbili.

Amesema, awaliwagonjwa hao walikuwa akipelekwa Nchini India kwa gharama kati ya Sh. 30 hadi 100Milioni.

Na kwamba, kwa sasa upankizaji huo unapofanyika hapa nchini serikali inagharamia Sh 21 milioni.

“Pia magonjwa yasiyoambukizwa kama vile Pressure na kisukari nayo anakuja juu kwani yanaongezekoa la wagonjwa na pia yanaweza kuleta tatizo la Figo.

Amesema, wakati umefika sasa kwa watanzania kujenga tabia ya kupima afya zao ili kujua hali ya miili yao.

Aidha asilimia 10 ya Watanzania wana afya iliyopitiliza kutokana na kutofanya mazoezi ya mara kwa mara.

Naibu waziri huyo amesema, unene siyo sifa kwani unahatari kubwa kiafya na hasa kama mtu afanyi mazoezi.

Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Afya ya Figo kwa kila mmoja na kila pahala”

error: Content is protected !!