Thursday , 2 May 2024
Home Kitengo Michezo Manara: Jumamosi ‘DO or DIE’
Michezo

Manara: Jumamosi ‘DO or DIE’

Spread the love

KUELEKEA mchezo wa klabu bingwa barani Afrika dhidi AS Vital kutoka nchini Congo, msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara amewataka mashabiki wa klabu hiyo kujitokeza kwa wingi siku hiyo ili kuweza kutoa hamasa kutokana na umuhimu wa mchezo huo. Anaripoti Faki Sosi.

Mchezo huo wa kundi D utachezwa siku ya juma mosi, 16 machi kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambao utakuwa ni wa mwisho na timu yoyote itakayo fanikiwa kushinda itakuwa imefuzu kwenda hatua ya robo fainali.

Akizungumza leo na waandishi wa habari, Manara amesema kuwa ili washinde ni lazima  mashabiki na wanapenda soka wazalendo wahamasike kwenda uwanjani kuishangilia timu hiyo na kukiri kuwa AS Vital ni timu nzuri.

“Tunawaomba tujaze uwanja kuhanikiza, tushangile , tuzomee,….kuanzia leo hakuna habari nyengine mimi ninao uwezo wa kuhamisha mazungumzo ya nchi hakuna stori nyengine labda afe mtu mkubwa … “ alisema Manara

“Nchi mzima tunaelekea taifa wiki hii yote hakuna stori yoyote stori ni moja tu tukishafanya hivyo, taifa hatoki mtu na ili tutoke na ushindi ni lazima tuhanikize, tushangilie, tuzomee, tukacheze hawatoki “ aliongezea msemaji huyo

Mpaka sasa Simba anashika nafasi ya mwisho kwenye kundi hilo akiwa na alama sita, nafasi ya tatu wakiwa As Vital wakiwa na alama saba sambamba na Al Ahly ambao wapo nafasi ya pili huku nafasi ya kwanza ikishikwa na JS Saoura mwenye point inane.

Kama Simba wakifanikiwa kushinda mchezo huo kwa idadi yoyote ya mabao watakuwa vwamefanikiwa kufuzu kwenye hatua ya nane bora licha ya kupoteza katika mchezo uliopita dhidi ya JS Saoura.

Katika hatua nyingine Manara alitangaza vingilio katika mchezo huo ambapo mzunguko itakuwa shilingi 3000, VIP B shilingi 10000, VIP A shilingi 20000, wakati huo tiketi za Platnum zitauzwa kwa shilingi 200000 na mchezo huo utachezwa saa 1 usiku.

Tazama video kamili hapo chini

https://youtu.be/5Uv0gPuoYB8

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Europa na Conference kukupatia pesa ndefu leo

Spread the love  ALHAMISI ya leo tutaenda kushuhudia mitanange ya kukata na...

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

Michezo

Usiku wa Ulaya umerejea kibabe kabisa

Spread the love  LIGI ya Mabingwa barani Ulaya imerejea tena na awamu...

Habari MchanganyikoMichezo

Mambo ya Ndani, Ulinzi zang’ara michezo ya Mei Mosi Arusha

Spread the loveRais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA), Tumaini...

error: Content is protected !!