Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Ajali mbaya yatokea Songwe, yaua abiria wote
Habari Mchanganyiko

Ajali mbaya yatokea Songwe, yaua abiria wote

Spread the love

WATU 19 wamepoteza maisha kutokana na ajali iliyotokea usiku wa kuamkia leo katika eneo la Senjele mkoani Songwe. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Akithibitisha kuhusu tukio hilo, Kamanda wa Polisi mkoani Songwe, SACP, George Simba Kiando amesema ajali hiyo iliyohusisha lori lenye namba za usajili T825 CMJ na gari la abiria aina ya Coaster (T269 CJC), ilitokea majira ya saa tatu na robo usiku.

Kamanda Kiando amesema chanzo cha ajali hiyo ni breki ya Lori kushindwa kufanya kazi katika mteremko wa mpakani mwa mkoa wa Mbeya na Songwe na kulikopelekea roli hilo kuigonga Coaster iliyokuwa na abiria 18 na kusababisha vifo hivyo.

Ameeleza kuwa, watu 17 akiwemo dereva wa roli walifariki papo hapo wakati wawili walifariki dunia wakati wakipatiwa matibabu kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mbeya.

Kamanda Kiando amesema katika vifo hivyo, watu 14 walikuwa wanawake na 5 walikuwa wanaume.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!